BENKI ya NMB imetoa viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwenye Shule ya Sekondari ya Mwanalugali kwa ajili ya kupunguza changamoto za shule hiyo.
Akikabidhi viti na meza hizo Mjini Kibaha Mkaguzi wa ndani wa benki hiyo Benedicto Baragomwa wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Mwanalugali amesema lengo ni kuboresha mazingira ya elimu.
Baragomwa amesema kuwa mwaka jana NMB ilizindua asasi ya kiraia inayoitwa NMB Foundation ambapo kuna kitu kinaitwa Nuru Yangu Scholarship na Mentorship Program ambayo inatoa ufadhili wa masomo ambapo kwa mwaka huu watafadhili wanafunzi 200 wa elimu ya juu na vyuo.
"Ufadhili huu ni wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kwa wale wanaoingia vyuoni kigezo kikubwa uwe umefaulu vizuri na pia wanaotaka familia duni,"alisema Baragomwa.
Alisema kuwa amani kuwa wahitimu wote hawa wataendelea na masomo katika vvuo vikuu washike masomo na wasome kwa bidii sana vijana kwani siku hizi vijana wamejenga dhana kuwa elimu bora inapatikana nje ya nchi yaani majuu ambapo hiyo ni dhana potofu, elimu ya Tanzania ni bora sana na tujivunie.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Joseph Mkumbo alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kutokuwa na uzio hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi hasa wavulana kutokana maeneo mengi kutoendelezwa na kusababisha matokeo kuwa mabaya.
Mwisho.
0 Comments