Mtandao wa Mange Kimambi wa Mange Kimambi App umetoweka hewani mchana wa leo Aprili Mosi huku awali mmiliki wa mtandao huo akieleza kuwa, itarejea hewani muda wowote, hata hivyo, majira ya saa tatu usiku dakika kadhaa zilizopita ameweka ujumbe juu ya kutoweka kwa App hiyo.
Katika andiko lake kwenye kurasa hiyo ya Instagram ya mangekimambi_ aliandika;
‘’Hi guys,
So hakukuwa na hacker yoyote yule ila kulikuwa na inside job. Yani ni mtu niliemwamini na kumpa access ndo aliedelete kila kitu.
Baada ya sisi kurudi online tu aliingia kwenye account yangu ya AWS na kufuta backups na akadelete mpaka server.
So haikuwa hacker but rather one of my TANZANIA developers.
Which is why sikutaka kudeal na developers watz tokea mwanzo… They are untrustworthy. Ila mlinilazimisha sana weka na developers wa kibongo, ningebakigi na wahindi wangu tu.
Anyways, tutakuwa down for 2-3 weeks . Tukirudi tutatoa 1 month free for everyone. Na tutarudi na moto wa kushinda mwanzo.
For now nafikiria kuweka a free channel ya telegram ili muendelee kula ubuyu kwa hizi wiki mbili tatu wakitengeneza tena.
Wanasema hakuna pesa rahisi, ndo hii sasa. Hata pesa ya umbea ni ngumu vile vile. Shughuli yoyote inayoingiza pesa nyingi lazma iwe na challenges lazma watu wahangaike kukuharibia.
Tutakaa sawa na umbea utaendelea vile vile.
Aliandika Mange Kimambi, hata hivyo, Matukio Daima App awali ilishuhudia moja ya bandiko la mwanadada huyo likituhumu moja ya idara nyeti hapa nchini kuwa inamtaka kufunga App hiyo. Hata hivyo bandiko hilo lililodumu kwa dakika 15 kwenye kurasa wake huo na kisha aliweza kuiondoa.
App hiyo iliyokuwa ya habari, ilijikita zaidi kuandika habari za umbea na matukio mbalimbali ikiwemo habari za Kitaifa na Kimataifa huku akitumia neno la ‘’ACHAFUA HALI YA HEWA’’
Hata hivyo, hivi karibuni alipata misukosuko na Jeshi la Polisi kwa kushikiliwa kwa wafanyakazi wake 13 ambao wawili waliachiwa hii leo walikuwa wakishikiliwa tangu Machi 14, mwaka huu kwa kosa la kurusha maudhui yasiyofaa mtandaoni ambapo ilidaiwa kuwa walirusha maudhui ya video ya Msanii na Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay.
Maudhui hayo yalidaiwa kuwa yalionesha Prof. Jay akiwa kitandani chumba cha wagonjwa mahututi [ICU] hali ambayo ilileta taharuki kwa ndugu wa mgonjwa, Madaktari na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa na kupatiwa matibabu.
Mtandao huu wa Matukio Daima ndo ulikuwa wa kwanza kuripoti juu ya tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi hao wa Mange Kimambi App zaidi ya 10, ambapo hata hivyo awali Jeshi la Polisi halikuwa wazi kusema hadi pale Mwanadada huyo kuandika kwenye kurasa wake ndipo taarifa ya jeshi ilitoka kwa umma juu ya kuwashikiria wafanyakazi 13 pamoja na vifaa vya ofisi mbalimbali zikiwemo camera, Laptop, na vingine vingi vya Kimawasiliano.
0 Comments