Header Ads Widget

MAAFISA UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO TEMBEENI KIFUA MBELE-DKT ABASI


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

MAAFISA Utamaduni,Sanaa na Michezo kote nchini wametakiwa kutembea kifua mbele kwani Wizara wanayoifanyia kazi ni ya kada ya kimkakati na hakuna nchi isiyokuwa na utamaduni wake hasa katika zama hizi za utandawazi.


Akiongea leo April 4,2022 jijini hapa katika kikao cha 13 kikao kazi Cha Maafisa utamaduni na michezo Tanzania bara Katibu Mkuu Dkt Hassan Abbasi amesema kukutana kwao huko ni njia mojawapo ya kuhakikisha utamaduni unalindwa Ili vizazi visije kuiga tamaduni za nchi nyingine huku akiwasisitiza kukikuza kiswahili.


Amesema wamekutana katika kipindi muhimu kwani kuna changamoto kubwa ya namba gani tutajifunza tamaduni za wengine na mnadhani tutaweza kulea na kuenzi tamaduni zetu, kikao hiki tunakutana katika Kipindi Cha kimkakati kwani tutaweza kutazama mambo gani ya kimaadili na tamaduni zetu tunazoweza kusimimia na kuenzi Mila na desturi zetu.


"Tunashuhudia mabadiliko makubwa kwa vizazi vyetu kuanza kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau kabisa tamaduni za kwao na hiyo yote inakuja au inachangiwa na utandawazi," amesema Dkt Abbasi.


Na kuongeza"Lakini pia tuhakikishe tunalinda na kukuza lugha yetu ya kiswahili kwani ni ukweli uwazi tujivunie lugha hii adhimu kutokana na kwamba lugha ya kuswahili ni nyepesi tofauti na lugha nyingine,"amesema.


Kwa Upande wake Aldof Adili Afisa Michezo Mkoa wa Dar es saalam amesema katika siku 360 za Rais Samia Suluhu Hassan Mambo makubwa Sana katika tasnia ya Michezo na utamaduni yametokea kwani serikalli imeweka fedha nyingi kwa ajili ya uendeshaji wa shule 56 za Michezo .


Naye Titto Lulandala Mwenyekiti wa Maafisa Utamaduni na Sanaa Tanzania wamekuwa na utaratibu wa kukutana wale watekelezaji wa sera za Kisekta wanaotekeleza majukumu yao katika ngazi mbalimbali za kitaifa ikiwemo  mikoani na wilayani wanaakutana na kuangalia changamoto na kujiwekea malengo ya baadae na ni utaratibu serikalli imekuwa ikiutekeleza kupitia Wizara hiyo ya kisekta  .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI