Header Ads Widget

KIKWETE AKEMEA VITENDO VYA RUSHWA WIZARA YA ARDHI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

NAIBU Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa Wizara hiyo  kupinga vitendo vya rushwa kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya Wananchi juu ya Baadhi ya watendaji na Maafisa Ardhi kujihusisha na vitendo hivyo.


Ameyasema hayo Leo Jijini hapa wakati akifungua mkutano wa Baraza  Wafanyakazi wa Wizara  hiyo, ambapo amesema rushwa ni adui wa haki na katika maeneo mengi Watu wamekuwa Wakilalamika sana kwa kuombwa rushwa kwa watendaji na Maafisa wetu 


"Sisi Kama watendaji wa Wizara tumekuwa tukikemea lakini Kama tunavyofahamu binadamu tumeumbiwa kusahau lakini tumekuwa tukikumbushan kwankusema hata kiongozi wetu Mkuu was nchi na maelekezo yake anaichukia rushwa na hataki itawalekatika Ofisi zetu,"amesema


Pia amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa kuzingatiwa utoaji wa haki kwani eneo hilo pia limekuwa likilalamikiwa kwa watendaji na Maafisa kufanya kazi bila kuzingatiwa utu na utoaji wa haki.


"Hivyo tumeendelea kuwasisisitiza wataalamu wetu kunambo mengi yanyotakiwa kurekubishwa hasa wanapo kwenda kupima maeneo ya Wananchi ni muhimu kuzingatia kuwawanakwenda kupima maeneo ambayo tayari watu wanayangalia hivyo wamiliki wa eneo wapewe kipaumbele ili kuondokana malalamiko yasio ya lazima," amesema


"Nasisitiza ondoeni uonevu katika utendaji kazi hasa Mfumo kandamizi katika usimamizi wa Mpango wa Ardhi ,mfano zoezi la upimaji linapofanyika kwa makubaliano ya kuchukuwa asilimia fulani ya viwanja kwa Wananchi lakini wakati huo huo kuwachaji tena Wananchi kulipa gharama za upimaji," amesema


Hata hivyo amewataka watendaji hao kutumiana nguvu Kubwa kwa kuujulisha umma Wizara inafanya nini ili watu wajue Serikali yao ya awamu ya Sita inafanya mambo gani katika eneo la Ardhi kwani kuna mambo makubwa yanakwenda kufanyika katika nchi hii ikiwemo kuhakikisha nchi inapimwa yote na zile taarifa zinazopatikana kwenye upimaji Mfumo wa kidigitali.


Amesema hali hiyo itawalahisishia Wananchi kutambua mtu kwenda sehemu furani au kujua Hati ya umiriki wa ardhi iko hai au imekufa Basi wasiwe na sababu ya kufiki maofisini na kukutana na ulasimu ambao baadae utawaingiza kwenye matatizo ya kutakiwa kutoa rushwa.

Hata hivyo Baraza hilo Pamoja na masuala mwengine wamejadili makisio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mwaka 2022/2023 ikiwani hatua muhimu kuelekea kuwasilishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi bungeni Jijini Dodoma.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI