Na Fatma Ally Matukio Daima APP, Dodoma
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali kupitia wizara ya ujenzi na uchukuzi iko tayari kushirikiana na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) endapo kutatokea changamoto yoyote katika utekelezaji wa jukumu ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati alipokua akifunga kikao cha Baraza la wafanyakazi wa TMA, huku akiitaka Mamlaka hiyo iainishe bajeti na njia za ukusanyaji wa mapato ili kuiwezesha taasisi kujiendesha kwa ufanisi.
Aidha, amewapongeza wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuendelea kufanya kazi vizuri na kutekeleza majukumu kwa ufanisi mkubwa licha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Nimeelezwa kuwa mmekuwa mkitekeleza vyema takwa la kisheria, hivyo nawapongeza sana, nimefurahi kusikia kwamba Baraza hili lina wajumbe kutoka vituo vyote vya Hali ya Hewa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia muundo wa mkataba wa Baraza lenu"amesema Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, amesema kuwa Mamlaka imehakikisha viwango na taratibu za kimataifa za utoaji wa huduma za hali ya hewa pamoja na usimikaji wa vifaa na mitambo vinazingatiwa.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, Mamlaka inafanya udhibiti wa shughuli kuu tatu ambayo ni uangazi wa hali ya hewa (meteorological observation), utabiri wa hali ya hewa (weather and climate forecasting) pamoja na kubadilisha mwenendo wa hali ya hewa (weather modification).
Ameongeza kuwa wamefanikiwa kuendelea kumiliki Cheti cha utoaji huduma bora ISO 9001:2015 ambapo katika ukaguzi wa kimataifa uliofanyika mwaka jana Disemba, 2021 Mamlaka ilifanya vizuri katika ukaguzi huo na hakukuwa na hoja ya ukaguzi (Non – Confirmity).
Hata hivyo, amesema kuwa wanaendelea na taratibu za ununuzi wa Rada nne (4) za hali ya hewa zitakazofungwa katika Mikoa ya Mbeya, Kigoma, Dodoma na Kilimanjaro.
Sambamba na hayo amesema malipo ya awali yameshafanyika na Rada hizo zinaendelea kutengenezwa huko Marekani, Rada hizo zinatarajiwa kufungwa kati ya mwezi wa Julai, 2022 na Juni, 2023, ukamilishaji wa mtandao wa Rada za hali ya hewa utasaidia utoaji wa huduma kwa Umma na kwa sekta binafsi na pia kuboresha .
0 Comments