Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI
Chama kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU)kimeelezwa ni sawa na sikio la kufa ambalo halisikii dawa kwani badala ya kubuni miradi ya kimaendeleo kupitia maeneo yake kama ilivyoolekezwa na serikali kimeitumia ardhi yake katika uwekezaji unaokinzana na sheria ya maendeleo ya biashara katikati ya mji(CBD)imebainika.
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa wizara ya kilimo Gerald Kusaya mara kadhaa alikishauri chama hicho kikongwe kutumia maeneo yake kutafuta wawekezaji ambao watajenga majengo makubwa ambayo yatatumika kama vitega uchumi kati kati ya mji kwa manufaa ya siku zijazo badala ya kusubiria biashara ya kahawa pekee.
Kinyume cha ushauri huo KNCU ikatumia ardhi yake iliyopo katikati ya mji(zilizopo ofisi za makao makuu za chama hicho) kwa kuruhusu ujenzi ambao sii wa ghorofa kama sheria ya mipango miji inavyoelekeza jambo ambalo lilipewa baraka na aliyekuwa meya wa manspaa ya Moshi Juma Rahibu ambapo kwa sasa uwekezaji huo licha ya kuwa unakiingizia mapato chama hicho ila hauendani na thamani ya ardhi na eneo lilipo na pia unakinzana na taratibu za ujenzi.
"Tulitamani sana hili eneo ambalo KNCU wamempa mwekezaji pangejengwa ghorofa kama sheria inavyoelekeza lakini imekuwa ni kinyume kwa maana nyingine hawa hawafikirii kwenda mbele na badala yake ni sawa na kuturudisha sisi manispaa nyuma"kilidokeza chanzo kutoka ofisi ya mipango miji
Hata hivyo sheria za uendelezaji wa maeneo ya kibiashara katikati ya mji(CBD)zimewekwa bayana kuwa hakutakuwa na jengo lakudumu ambalo litakuwa sii ghorofa na kuwa kama mmiliki wa kiwanja hana uwezo wa ujenzi wa ghorofa ajenge nyumba ya chini na kuacha matoleo ambapo atakuja kuendelea siku zijazo.
Inadaiwa kutokana na ombwe la kiuongozi lililokuwepo likiongozwa na Juma Rahib aliweza kutoa kibali cha ujenzi wa jengo katika eneo hilo jambo ambalo ni kinyume cha taratibu na kuwa sasa tayari suala hilo lipo mikononi mwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)kubaini uhalali wake.
"Tumepokea tuhuma nyingi kuhusiana na aliyekuwa meya (Juma)ikiwemo utoani wa vibali vya ujenzi visivyoruhusiwa ila kwa sasa ni mapema sana tupo tukiwa tunazifanyia uchunguzi na zikiwa tayari mtajulishwa tu"mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro Frida Wikes
Godfrey Massawe ni kaimu meneja mkuu wa KNCU ambapo kwa siku tatu mfululizo kila alipotafutwa kwa njia ya simu kutoa ufafanuzi juu ya uhalali wa uwekezaji huo usioendana na sheria za mipango miji alijibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa yupo kwenye kikao.
Aliyewahi kuwa meya wa manspaa ya Moshi Jaffary Michael alisema katika kipindi cha utawala wake hakuruhusu ujenzi holela usiofuata taratibu za mipango miji jambo lililojenga taswira nzuri ya mji lakini ghafla ndani ya miaka michache nyumba zikaanza kuota kama uyoga.
"Hizi sheria za kutoa vibali vya ujenzi zipo wazi kabisa lakini kwa kuwa kuna kikundi cha watu wachache waliona ni fursa ya upigaji basi mambo ndio kama haya unayoyaona sasa hapa katikati ya mji"alisema
Mwanzoni mwa wiki hii aliyekuwa meya wa mansipaa ya Moshi Juma Rahib aling'olewa katika wadhfa wake huo kwa kupigiwa kura 18 za hapana kati ya 28 na madiwani wakimtuhumu kwa mambo mbalimbali ikiwemo kujihusisha na matumizi mabaya ya ofisi.
Tuhuma nyingine ambazo alihusishwa nazo na yeye kukiri kupitia tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa ni pamoja na kutoa vibali vya ujenzi kiholela huku akipokea kiasi vha fedha(milioni 2-3) pamoja na kuhudhuria hafla ya siku ya kuzaliwa kwa kijana mmoja anayejihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja(shoga)
0 Comments