NA HADIJA OMARY _LINDI.....
JUMLA ya viwanja 4383 katika Wilaya za Mkoa wa Lindi vimefanyiwa urasimishaji wa kupimwa kufuatia zoezi la upimaji wa maeneo uliofanywa ofisi ya Aridhi Mkoani humo
Zoezi hilo ambalo lilianza mwezi February 20202 lina lengo la kuwapatia hati miliki za maeneo yao ambazo zitawasaidia kukopa kwenye taasisi za fedha.
Akizungumza na matukio Daima Afisa aridhi kutoka ufisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw.Kaseja Minga alisema kuwa limefanyika kwa kushirikiana na wananchi wenye maeneo hayo na kwamba halite husisha ubomoaji wa majengo yao
Alisema kwenye zoezi hilo la upimaji wale wote ambao wanazo hati miliki za viwanja vyao hawataguswa kwenye zoezi hilo
Hata hivyo Bw. Minga alisema kwa pamoja na zoezi hilo wameweza kutatua migogoro 27 ya Aridi iliyokuwa inawakabili wananchi hao katika maeneo yao
Aidha pamoja na mambo mengine Bw. Minga amewataka. wananchi kulipa Kodi ardhi Kwa wakati ilikuepuka usumbufu ikiwemo kunyangangwa Ardhi. Lindi..
Mtaa wa Mitwero Manispaa ya Lindi Mkoani humo ni miongoni mwa Maeneo yaliyofikiwa na zoezi hilo ambapo Wananchi wa wameipongeza Serikali kwa kuanzisha zoezi la upimaji viwanja (urasimishaij)kwa gharama nafuu kwa ajili ya kuwapatia hati miliki.
Wananchi hao wamesema maeneo hayo wanaishukuru Serikali kwa kuanzisha utaratibu wa urasimishaji na kwamba gharama za upimaji ambazo ni 130,000 watailipa bila shida.
Amina selemani mkazi wa mtaa wa mitwero amesema utaratibu ulioletwa ni mzuri kwani awali walikuwa wakitumia gharama kubwa, hivyo wamepata matumaini mapya watapimiwa viwanja vyao na kupatiwa hati miliki na wataweza kukopa kiurahisi na kufanya biashara ili kujiendeleza kiuchumi.
Mpango huu tumeupokea mikono miwili kwani tunaamini kiwango kilichowekwa Wananchi wanauwezo nacho tutalipia fedha"amesema Amina
Juma musa amesema kuwa mpango ni mzuri ila ameiomba serikali kuharakisha zoezi hilo na lifanyike Kila wilaya kwani itaweza kupunguza migogoro ya Ardhi nchini.
"Tatizo la migogoro ya viwanja ni la muda mrefu hivyo kuwepo kwa mkakati huu utasaidia kutatua migogoro amesema Juma
0 Comments