Header Ads Widget

WANANCHI MTAMA WAJIFUNGULIA NJIANI KWA KUKOSA HUDUMA ZA AFYA


Licha ya Sera ya Afya kuelekeza kila Kijiji lazima kiwe na Zahanati lakini bado wakazi Zaidi ya 5000  wa kata ya Navanga Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wamejikuta wakitembea umbali mrefu wa Takribani kilometa tisa kufuata huduma hiyo hali inayopelekea akina mama kujifungulia njiani .MWANDISHI HADIJA OMARY MDTV LINDI

Pamoja na kwamba wataalamu wa Afya wanasisitiza kuwa ni  muhimu kwa mama anapohisi tu mjamzito kuhudhulia kliniki ili kuweza kupata chanjo na ushauri lakini hali hiyo ni tofauti kwa akina mama wa Navanga ushindwa kufanya hivyo kutokana na gharama kubwa ya usafiri wanazotumia wakati wakifuata huduma hizo

Akizungumza na Mtukio Daima Issa Chande Mkazi wa Navanga alisema kuwa kutokuwepo kwa huduma hiyo Afya  katika maeneo yao kunapelekea akina mama kushindwa kuhudhuria kliniki kwa wakati pindi wanapokuwa wajawazito na wengine kujifungulia njiani wakiwa wanafuata huduma hiyo


“ tuna miaka mingi hatuna Hospitali Navanga, huduma inakopatikani ni Nachunyu mimi mwenyewe ninaezungumza mke wangu aliwahi kuwa na Ujauzito aliwahi kujifungulia njiani wakati tunaelekea kwenye hiko Kijiji cha jirani hata hivyo kulingana na huduma alizohitaji tulilazimika kutoka katika hospitali hiyo ya Nachunyu kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lindi Sokoine kwa ajili ya Matibabu Zaidi”

Nae Ashura Salamu Mkazi wa Navanga alisema  kwa  kuwa huduma za Afya zinapatikana mbali na maeneo yao ulazimika kutumia sio chini ya shilingi elfu 5000 kama nauli ili kuzifikia huduma hizo jambo ambalo kwa Maisha ya sasa inakuwa ni ngumu. 

“uwe na hela ya kulipia nauli , uwe na hela ya kulipia huduma na hali ya sasa ilivyokuwa ngumu tunashindwa . utakuta mtu anaenda kuanza kliniki miezi michache ya mwishoni au asiende kabisa jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto alie tumboni”

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Rashidi Mkuya alisema kuwa kwa kutambua changamoto wanazokabiliana nazo wakazi wa kata hiyo hasa katika vijiji vya Navanga, Nampunga na Mongo Mongo wananchi wenyewe wameona ipo haja ya kujitolea kwa nguvu zao kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika Kijiji Cha Navanga ambayo itakuwa katikati ya vijiji hivyo ambavyo vimekosa huduma za Afya ambao kwa sasa umefikia hatua ya boma la kozi kumi

Kwa upande wake  Mganga Mkuu Wa Halmashauri ya Mtama  DKT, Dismas Masulumbu  amekili kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo alisema kuwa kata ya Navanga ni miongoni mwa vijiji vitano  vilivyopo katika halmashauri hiyo ya Mtama ambavyo Wananchi wenyewe  kwa kutambua umuhimu wa huduma za Afya wameanzisha ujenzi wa Zahanati ambao umefikia katika hatua mbali mbali za umaliziaji

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni pamoja na Navanga, Nauka uka A, Nauka uka B, Ruhokwe na Ntene ambayo mpaka sasa wanasubiri fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji ambao utafanywa kwa kipaumbele kulingana na hatua ya jingo ilipofikia

Hata hivyo pamoja na kuwapongeza Wananchi wa maeneo hayo kwa jitihada walizozionyesha za kuanzisha ujenzi huo wa zahanati pia alitoa wito kwa wananchi hao kuendelea kushirikiana katika kuendeleza ujenzi huo ili uweze kusogea mbele Zaidi 

Hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa Zahanati hiyo kupitia  Mkutano wa Mfuko wa jimbo wenye lengo la kugawa fedha za maendeleo kwenda kuchochea shughuli mbali mbali kilichoongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo , Waziri wa Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nnauye    umetenga jumla ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati hiyo 

Ili Mtoto aweze kukua vizuri swala la Afya kabla na baada ya kuzaliwa  ni miongoni mwa mambo matano muhimu yaliyotajwa kwenye Program jumuishi ya  Taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali yam toto (PJT-MMMAM)  


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI