Header Ads Widget

WAGANGA WAKUU WA MIKOA WAJIFUNGIA DODOMA KUJADILI CHANGAMOTO YA DAMU SALAMA NA DAWA


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma 

NAIBU Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amekutana na waganga wakuu wa Hospital lengo likiwa ni kujadili changamoto iliojitokeza ya uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya hapa nchini.


Kikao hicho maalumu kilichofanyika jijini hapa ambacho kililenga kujadili changamoto juu ya Masuala ya damu salama na upatikanaji wa dawa sehemu zote za kutolea huduma.


Pia amewataka waganga wakuu hao kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya kwani ndio kipaumbele cha Wizara ni kuona huduma za afya kwa Wananchi zinakuwa bora. 


"Nendeni mkaboreshe Huduma kwa wateja (Customer Care) na kukua ni namna gani mnazungumza na wateja kumbukeni si kila wagonjwa wanaokuja kwenye vituo vya Afya wanahitaji dawa wengine wanahitaji kutiwa moyo na ushauri nasaha na kupewa matumaini," amesema Dkt Mollel.


Kwa Upande wake Japhet Simeo mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita na Katibu wa Umoja wa Waganga wa Kuu wa mikoa Tanzania bara akiongea kwa niaba ya waganga wakuu wa mikoa amesema kumejitokeza uhaba Mkubwa wa damu na hali hiyo imekuja baada ya huduma za afya kupanuliwa au kusogezwa karibu na wananchi.


Amesema Serikali ya awamu ya Sita imefanikiwa  kupanua huduma kwa kiwango kikubwa  kwa Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zaidi ya 100 zimeweza kujengwa na kukamilika huku nyingine zikianza kutoa huduma.


"Sehemu Kubwa inaonyesha wananchi  Sasa wanakwenda hospitalini kutibiwa pindi wanapougua na hata tafiti zinaonyesha Wananchi wengi walikuwa wakienda kutibiwa katika tiba mbadala baada ya huduma kusogezwa karibu na wananchi na ndio maana wananchi wanakimbilia huduma hospitalini hali inayopelekea uhaba Mkubwa wa damu na dawa katika Vituo vya Afya.

Aidha amesema Ajenda ya damu salama na upatikanaji wa dawa ndio kitu muhimu katika huduma na Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya dawa lakini kadri siku zinavyozidi kwenda mapungufu yanaonekana kutokana na Wananchi Kwenda kupata huduma katika vituo vya Afya.

Hata hivyo amesema changamoto ni rasilimali fedha zitakazoweza kuwasaidia kupata vifuko vya kukusanyia damu na jinsi ya kuwafikia wananchi Ili kuwapa vipeperushi ya kutoa elimu juu ya kujijengea utaratibu wa kutoa au kuchangia damu.

Naye Dkt Magdalena Lyimo Meneja wa Mpango wa Taifa wa damu Salama amesema wamekutana katika kikao muhimu lengo Ni kuhakikisha huduma za damu Salama inapatikana muda wote pia huduma za Afya zitolewe kwa usahihi na zenye tija

Amesema Shirika la Afya duniani(WHO) linapendekeza Ili kukidhi mahitaji ya damu ya nchi inabidi kukusanyia chupa ambazo idadi yake ni sawa na asilimia moja ya Wananchi ambao wapo kwenye nchi na Tanzania tumeweza kukusanya chupa laki 5.5. Tutakuwa tumefikia mahitaji ya nchi.

Mwaka Jana mwaka wa fedha 2020 /2021 walikusanya chupa 330,000 ambayo ni asilima 60 na ambapo kuna pengo la asilimia 40 na ndio maana tuko japo iliwekwa mikakati madhubuti kuhakikisha pengo Hilo linafutika na chupa hizo laki 5.5 zinapatikana .

"Ni muhimu kuwa na damu Salama na ya kutosha katika Vituo vyetu vya Afya kwani wamama wajawazito wamekuwa wakipoteza damu nyinyi wakati wa kujifungua na watoto wenye Umri chini ya miaka 5 wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuishiwa damu,na tatizo hilo limekuwa likitibiwa kwa kuongezewa damu.

Kwa Upande wa majeruhi wa ajali bila kusahau Sekta ya Afya Huduma za Afya zimeboresha Sana nchi inakwenda kutoa huduma za kibingwa na Bobezi ikiwemo upasuaji wa kitaalamu na hizo zote inategemea damu ya kutosha na salama.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI