Header Ads Widget

TAKUKURU DODOMA YAANZISHA KAMPENI MAALUM YA ULIPO TWAJA.

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma 


TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imeanzisha kampeni maalum ya uelimishaji ya "ULIPO TWAJA" ambayo uwafuata wananchi waliopo kwenye mikusanyiko na kuwaelimisha masuala ya ubadhilifu na rushwa ambapo hadi sasa wananchi takribani 45,000 wameelimishwa kwenye mikusanyiko 88 ndani ya mkoa wa Dodoma .


Amesema mkoa wa Dodoma unakadiriwa kuwa na wakazi 2,729,153 na kwamujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 asilimia 52.2 ya watanzania ni wale wa rika la miaka 15 hadi 64 hivyo katika kampeni hiyo ya ULIPO TWAJA Takukuru Mkoa wa Dodoma imekusudia kuwafikia angalau asilimia 10 ya wananchi wa rika hilo ambao ni takribani wakazi 142,461.


Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema uelimishaji huo uloanza januari 18 mwaka huu unalenga kuwafikia wananchini ambao wapo kwenye mikusanyiko mbalimbali.


Mkuu huyo amesema Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuzuia na kupambana na ubadhilifu wa mali za umma badala ya kusubiri hadi zifujwe ndipo uchunguzi ufanyike .


Ameeleza kuwa wao kama Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa wameona uelimishaji huo ni sahihi kwani utawafikia wananchi wanatumia muda mwingi katika shughuli za kujipatia riziki zao masokoni,Vituo vya bajaji na bodaboda vijiwe vya kahawa au wale ambao wanaenda kupata huduma kama mikusanyiko ya wanufaika wa TASAF, siku za lishe kwenye Vituo vya afya, siku za kliniki au chanjo,stendi za daladala na mabasi,Nk.


"Lengo la kampeni hii ni kuwafikia wananchi ambao kulingana na aina ya kazi au Biashara wanazofanya sio rahisi kuwapata kwenye mikutano ya hadhara au mikutano mingine rasmi kama ya Vijiji na Mitaa inafahamika wazi wengine uendeshaji wa maisha yao hutegemea uwepo wao katika maeneo hayo yamikusanyiko hivyo sio rahisi kuondoka na kuacha shughuli zao ili wahudhurie mikutano ya hadhara ,"amesema Kibwengo.


Aidha amesema  iwapo mkusanyiko husika utakuwepo saa 12 asubuhi  basi ULIPO TWAJA itawafuata na kuwaelimisha hata kama mkusanyiko  huo utakuwa mchana au njioni .


 Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI