Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA KAGERA WAPEWA ELIMU JUU YA MFUMO MPYA WA KIELETRONIKI WA RITANI YA VAT.



Na, Titus Mwombeki- MTDTV BUKOBA.


Wafanyabishara  mkoani Kagera wametakiwa  kukaa tayari kwaajiri ya kuanza kutumia mfumo mpya wa uwasilishaji wa  mfumo  mpya wa kielekroniki  wa ritani  unaotegewa kuanza kutumika mwanzoni mwa mwezi wa Machi  mwaka huu.


Kauli hiyo  imetolewa na afisa huduma wa  TRA mkoa wa kagera Alex Mwambenja wakati akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Manispaa ya Bukoba   namna ya kutumia mfumo huo utakao saidia   kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo wafanyabishara kupigwa faini pindi wanapochelewa kulipa kodi kwa wakati kwa sababu mbalimbali. 


“ Tumewaomba wafanyabiasha kuwa na kompyuta ambazo zinatumia mfumo wa ‘exel’ ya kuanzia 2010 hii itawasaidia kuwasilisha ritani kwa usahihi zaidi, tunawakumbusha pia wafanyabiashara waweze kuwasilisha makadilio yao yote ya mapato kabla ya tarehe 31 mwezi Machi ili kuepusha faini ambazo sio za lazima ambazo wanaweza kupiwa na TRA endapo watachelewa kutunza taarifa zao kwa wakati”




Amesisitiza kuwa, wafanyabishara wote hasa wale wanaofanya biashara kutoka nje ya nchi kuakikisha wanapoenda kununua bidhaa  wawekewe TIN zao wakati wa manunuzi.


“Mfanyabiashara yoyote ambaye hatawekewa TIN yake pamoja na namba ya kudhibitisha wakati wa manunuzi ya bidhaa yake, lisiti hiyo aitatumika kwenye madai ya kodi ya ongezeko la thamani”


Kwa upande wake Ibrahimu Sokwala ambaye ni mfanyabiashara katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, ameishukuru taasisi ya ukusanyaji mapato TRA mkoani kagera kwa utoaji wa elimu juu ya mfumo mpya wa kielekroniki wa uwasilishaji wa ritani ya VAT na kuwaomba TRA kuendelea kutoa semina kama hizi kwa wafanyabiashara kwani zinawasaidia kuongeza uelewa.



“Sisi kama walipakodi tunafurahi sana tunapopatiwa semina kama hizi, mfano wafanya biashara wengi kabla ya kupatiwa elimu juu ya mfumo huu mpya unaoenda kutumika  tulikuwa tunajiuliza maswali mengi hasa kama tutaweza kuumudu  lakini kupitia semina hii  ambayo tumepatiwa tumejifunza na kupatiwa majibu ya maswali mbalimbali ambayo yalikuwa yakitutatanisha”




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS