NA ANDREW CHALE.
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete anatarajia kufanya ziara maalum ndani ya jimbo hilo inayoanza leo Machi 2,2022 katika Kata ya Miono.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo hilo la Chalinze imeeleza kuwa, anatarajia kuanza ziara hiyo katika Kata ya Miono ambapo atakuwa na mikutano Mitatu na kisha ataendelea Kata zingine.
"Kata ya Miono anatarajia kufanya mikutano maeneo ya Kweikonje, Masimbani na atamalizia Miono mjini.
Watu wote wanakaribishwa kuja kumsikiliza Mbunge wao lakini pia atatembelea miradi ndani ya Kata pamoja na shughuli za kichama." Ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, Kata zingine ambazo nazo atazitembelea kwa siku tofauti:
Siku ya Ijumaa Machi 4 atakuwa na mikutano Kata ya Vigwaza.
Ambapo atafanya katika maeneo ya Buyuni, Visezi na Vigwaza.
Lakini pia Jumamosi ya Machi 5, atafanyamkutano kwenye Kata ya Kibindu.
Ambapo atafanya mikutano maeneo ya Kwamduma, Kwamsanja na mwisho eneo la Kwakonje.
Aidha, anatarajiwa kufanya mkutano wa mwisho Jumapili ya Machi 6, katika Kata ya Msoga katika eneo la Diozile, Tonga na baadae atamalizia eneo la Mboga.
Katika mikutani hiyo pia anatarajiwa kuongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Kiserikali, Chama Cha Mapinduzi CCM.
0 Comments