Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima Media Dar.
Baada ya Matukio Daima Blog kuripoti kwa mara ya kwanza taarifa za Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliovamia ofisi za Mange Kimambi App zilizopo Mtaa wa Togo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, tukio lililotojea jana Machi 14,2022 na kukamatwa kwa wafanyakazi wake wote pamoja na kuchukuliwa na vifaa vya ofisi,
Tayari mmiliki wa Mtandao huo, Mange Kimambi mwanadada Mtanzania anayeishi nchini Marekani ameibuka na kuandika haya:
"Yes, mlichosikia ni kweli kabisa. @mangekimambi___app ofisi nzima watu zaidi ya 10 wako central toka jana asubuhi.
"Nna mengi ya kusema, yani nataka kuharisha haswa ila sasa inabidi nitumie akili maana nachosema kinaweza kuwapa shida.
"Wamefunguliwa kesi ya matumizi mabaya ya mitandao kutokana na ile clip ya Professor Jay. Wanataka kujua nani alienipa ile clip. Tatizo ni kwamba hao wafanyakazi hata wawachape viboko hakuna hata mmoja wao ataewapa jibu.
"Hata wawaeke ndani mwaka hakuna wa kuwapa jibu maana hawajuiiii. Mimi peke yangu ndo nina uwezo wa kuwaambia clip imetokea wapi ila mimi huwa nafuta chats zangu soon as nikifanyia kazi kuepusha sources zangu kujulikana iwapo ntapoteza simu
"It’s seems wanawashikilia wafanyakazi wangu kama kunikomesha mimi, ila tatizo ni kwamba mimi niko marekani nimeweka nne wanaokoma ni watoto wadogo, watoto ambao hawana hata impact yoyote na app, hao watoto wako ndani toka jana asubuhi na Mange Kimambi App onaendelea kama kawaida kilichokuwa affected kwenye App ni hard news na sports.
"Mpaka hapo ilibidi wajue wamewashikilia innocent people.
"So it seems wanataka mimi niwaambie nani kanitumia ile clip ndo hii kesi iishe ili waweze kudili na huyo mtu. Tatizo ni moja.
"1. Siwezi kumjua huyo mtu maana nilishadelete chats zetu.
2. Hata ningekuwa sijadelete chat bado nisingetaja nani kaniambia. Yani hata waifunge App , siwezi kusema sources zangu, nini kuwakamata wafanyakazi, hata nifanywe nini nisingemtaja aliesema.
" Bora nife kuliko kusema nani ndo aliniambia nini.
" Yani niko tayari app ifungwe nirudi kuwa jobless ila siwezi kumwaribia mtu mwingine maisha yake kwa kumtaja ili nijiokoea mimi.
"3. Na hao Muhimbili wanajipa headache bure wafanyakazi wao wamuhimbili wako innocent. Sikutumiwa ile clip na nurse, wala doctor wala mfanyakazi, clip imetumwa na friends/family.
"@policetanzania Kesi ya vijana wangu ina dhamana ila toka jana mnawanyima dhamana why??? Dhamana ni haki yao.
"Tanzania tulishapita hiyo stage ya kufanyia ubabe na kwenda kinyume na sheria.
" Wapeni vijana haki yao ya dhamana….." alimalizia Mange Kimambi ujumbe ambao alipost kwenye kurasa wake rasmi wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya Milioni 6.4.
0 Comments