







****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali imewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanaweka tahadhari zote ikiwemo za moto na kuendelea kuwa na bima ambayo itawasaidia pindi ikitokea itirafu yoyote kwenye kiwanda na kusababisha kupoteza mali zake waweze kufidiwa mara moja
Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe mara baada ya kutembelea kiwanda cha GSM kilichoungua hivi karibuni ili kujionea hitirafu iliyotokea.
Amesema baada ya uchunguzi kukamilika katika kiwanda hicho basi wapo tayari kuwasikiliza GSM kuona ninamna gani Serikali inaweza ikawasaidia ili uzalishaji uweze kuendelea.
"Hili ni pigo sio kwa GSM pekee bali kwa nchi nzima lakini pia kwa Serikali ambayo inapenda viwanda viendelee kuzalisha bidhaa muhimu ambazo zinatumika katika nchi yetu". Amesema
Amesema Serikali inawajibu wa kulea Sekta Binafsi hasa kwenye viwanda ili waendelee kuzalisha kwa tija, kutoa ajira na kuokoa fedha ambazo zingetumika kama bidhaa hizi zinazozalishwa na kiwanda husika zingeagizwa kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wa GSM wameshindwa kuzaungumza kwa maana wakisubiri Uchunguzi ufanye na baadae wataeeleza ni nini kifanyike na pia kutoa maoni yao kwa Serikali.
0 Comments