Kutokana na serikali kuendelea kuwajili na kuwathamini wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwajengea masoko ya kisasa ya kufanyia biashara zao.MWANDISHI CHAUSIKU SAID,MDTV,MWANZA.
Akizungumza katika kamati ya siasa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo ameeleza kuwa serikali imetoa sh, mil 5000, 000, 00 kwa ajili ya ujenzi wa soko la Machinga
Diallo ameeleza kuwa jumla ya masoko 48 yamepokea wafanyabiashara 18, 271 na wameishapatiwa maeneo ya kufanyia biashara katika Halmashauri zoe (8) za Mkoa wa Mwanza
"Kwa kuwa mji unazaana sana na kupanuka wilaya zote mbili ilemela na Nyamagana ni lazima kuwe na maeneo yatakayowawezesha wamachinga kupata sehemu husika ya kufanyia kqzi kwa urahisi" alisema Diallo.
Aidha ameeleza kuwa chama pamoja na serikali kimewaomba wamachinga kuendelea kuwa watulivu na wenye subira wakati huo mipango ya serikali kupata fedha ya kuwajengea masoko ya kisasa inaendelea.
" Mpaka sasa utayarishaji wa michoro na zabuni za ujenzi zinakamilishwa" Alisema Diallo.
Kwa upande wake katibu wa CCm Mkoa wa Mwanza Julius Peter ameeleza kuwa kutokana na mpango wa serikali ya awamu ya sita Madiwani wote wa Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela walienda Dodoma kujifunza namna walivyojenga masoko kwa ajili ya wafanyakazi wadogo wadogo.
" wamekwenda huko kujifunza na wamerejea na wanafanya vikao pamoja na mtaalam ambaye alibuni mchoro wa jengo la machinga huko jijini Dodoma" Alisema peter.
Peter ameongeza kuwa ni lazima kuwe masoko ambayo yatakuwa imara kwa ajili ya kufanyia kazi kwa wamachinga wote.
0 Comments