.
NA MATUKIO DAIMA DAR.
MIILI ya wafanyakazi wawili wa chuo Kikuu Mzumbe akiwemo Mkuu wa Ndaki ya Dar es salaam, Prof Prosper Honest Ngowi na dereva wake Innocent Mringo, inatarajiwa kuagwa siku ya Alhamis Machi 31 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro Kwa maziko.
Akizungumza kwa niaba ya Menejimenti ya chuo kikuu Mzumbe, Mkurugenzi wa mawasiliano wa chuo hicho Bi Rose Joseph, alisema halfa hiyo ya kuaga miili hiyo imelenga kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu hao kama watumishi wa umma na vile vile kama wanataaluma ambapo Mringo atazikwa Ijumaa nyumbani kwao Marangu Mwika na Prof Ngowi atazikwa Jumamosi kijiji cha Singa Kati Kibosho,Wilayani Moshi
Umauti wa wafanyakazi hao ulitokea asubuhi ya Machi 28,2022 kwa ajali ya gari eneo la Mlandizi Mkoani Pwani wakiwa njiani kwenda Kampasi Kuu Morogoro.
APP YA MATUKIO DAIMA INAPATIKANA BURE KABISA GOOGLE PLAY STORE
0 Comments