Header Ads Widget

MHE RIDHIWANI KIKWETE AKAGUA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI INAYOJENGWA KIJIJI CHA MSOLWA

 



Na Andrew Chale, Chalinze.



Mbunge Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua ujenzi wa shule ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Msolwa huku akiwataka wazazi kuhimiza watoto wa kike kupatiwa elimu ilikuwa na akina Mama Samia wajao.


Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo wakati wa leo  Machi 7, wakati wa kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji hicho eneo la Makondo mengi



 Ambapo amesema: "Mafanikio ya ujenzi wa Shule hii ya Sekondari Msolwa yanakwenda kuwezesha kuwapo kwa Wakinamama Samia wengi siku zijazo" alisema  Mh. Kikwete


Na kuongeza kuwa, Serikali inafanya juhudi kuhakikisha wanasogeza huduma muhimu ikiwemo hiyo ya shule ambapo itakuwa mkombozi kutokana na watoto wanaofaulu kwenda mbali kufuata shule za sekondari.


"Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Milioni 600 zilizowezesha ujenzi wa  Shule ya Sekondari ya  Msolwa," Alisema.



Ujenzi wa shule hiyo utapunguza kero ya wanafunzi kufuata huduma hiyo mbali kwani wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakiwemo watoto wa kike.


"Kazi Inaendelea Chalinze ili kuendana na kasi ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka Kazi Iendelee" alimalizia Mhe. Ridhiwani. 


Ujenzi huo naoendelea unatarajia kukamilika mwakani huku ikitarajiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Msolwa na Vijiji jirani



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI