TAZAMAMA VIDEO HII HAPA BOFYA LINK HII

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama,
JESHI la Polisi mkoani Kigoma laingia Katika kashfa nzito baada ya askari wake kutuhumiwa kuua mtu mmoja kwa kupigwa risasi na kujeruhi wengine wawili wakati polisi wakituliza vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa mpira wa miguu wa kombe la kumbukumbu ya Dkt. Livingstone katika uwanja wa Lake Tanganyika jana jioni
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho na watu wawili kujeruhiwa kwa risasi pamoja askari no F 5123 Kolpo Subira anayetajwa kujeruhiwa kwa kupigwa na jiwe, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema askari walilazimika kutumia nguvu ya ziada kutokana na ukubwa wa vurugu baada ya kupiga mabomu ya machozi na risasi hewani bila mafanikio.
Wakielezea tukio hilo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa Jeshi la Polisi lilitumia nguvu zaidi wakati fujo zilikuwa zimeshaisha na kulalamikia taarifa ya polisi kuhusiana na tukio hilo na askari aliyehusika
0 Comments