Header Ads Widget

KAMANDA LYANGA DODOMA NI SHWARI WAGENI KARIBUNI

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

KUFUATIA Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) naotarajiwa kufanyika April 1 ,2022 hadi  April 2 ,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amesema hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Dodoma ni salama na shwari na hakuna matukio makubwa ambayo yameweza kuvuta hisia na taharuki na wananchi wanaendeleea na majukumu yao kama  kawaida.

Akiongea leo Machi 31 ,2022 Kamanda Lyanga amesema kuwa Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe wengi na viongozi wakubwa  wandani na nje ya Nchi akiwemo Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo wajumbe hao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 3000.

"Tunajuwa wazi panapokuwa na matukio nakubwa kama haya kuna kuwa na baadhi ya watu wenye nio ovu wanaopenda kutumia nafasi kama hii ya kuwepo kwa wingi wa watu kama huu kufanya uhalifu," 

"Hivyo waelewe kwamba Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama tumejipanga vizuri kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na doria itakuwa kali katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma," amesema Kamanda Lyanga.

Aidha amewaomba wananch kufuata sheria pamoja na Kutoa taarifa za matukio yeyote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani pamoja na kuhakikishi wanaheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo kuheshimu misafara mbalimbali ya viongozi kama watakavyokuwa wanaelekezwa na askari barabarani. 

Hata hivyo kamanda huyo amewataka wahudumu wa nyumba za kulala wageni kuwapokea na kuwakarimu wageni pamoja na kuwawekea ulinzi na panapotokea changamoto yoyote ya uvunjaji wa amani kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwaajili ya kushughulikiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI