WAZIRI wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dk Doroth Gwajima amesema jamii inapaswa kutambua kuwa wanawake walibaki nyuma miaka mingi na sasa huu ni muda wao wa kuleta maendeleo.
Aliyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa tamasha la mwanamke wa Pwani la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani
Gwajima alisema baba utamwachaje mama watoto bila kumpa maendeleo akina baba wahamasisheni watoto wa kike.
Aidha alisema akinababa wasaidie watoto wa kike ili waje kuwasaidia hata baadhi akinababa wanapata magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutokana na kutokuwa na wa kukusaidia.
Alibainisha kuwa huu siyo muda wa kuona mabinti wanaozwa kwani wanapaswa kupatiwa elimu ndiyo sababu hata Rais aliona baadhi ya mabinti walikosa elimu na kuruhusu waliopata ujauzito na kujifungua waende shule kutokana na ukatili waliofanyiwa.
"Rais ni Nyota ya Pwani na tukizindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kitaifa tuombe lizinduliwe hapa Pwani ndiyo mmebeba ajenda hii kwani Rais ni mkombozi wa Wanawake kwani amefungua milango na dunia nzima inajua kutokana na umahiri wa kuiongoza nchi,"alisema Gwajima.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa Rais ameonyesha uwezo wa mwanamke katika ukombozi kwao.
Kunenge alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike wa mkoa wa Pwani wanapata elimu na hata kama akichezwa ngoma bado atapata elimu kwani mila na desturi ni muhimu ngoma siyo kweli ni majembe kwa sasa mila ha desturi ni muhimu lakini elimu ni muhimu zaidi.
Naye mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Farida Mgomi alisema kuwa wanawake wamenufaika sana na wanakila sababu ya kumshukuru Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.
0 Comments