Header Ads Widget

HALMASHAURI YA SONGEA DC YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUINUA TAALUMA KWENYE SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

 


Na Amon Mtega, Songea.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma imefanya uzinduzi wa mkakati wa kuinua Taaluma kwenye shule za Msingi na Sekondari za kwenye Halmashauri hiyo ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi.

  


Akitoa taarifa hiyo   juu ya uzinduzi wa mkakati huo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe amesema kuwa uzinduzi wa mkakati huo umefikia baada ya kutambua kuwa kwa miaka kadhaa ya nyuma Halmashauri hiyo haikufanya vizuri kwenye upende wa taaluma .


Mkurugenzi Maghembe akitoa taarifa hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge amesema kuwa mkakati huo utaisaidia jamii wakiwemo na wadau mbalimbali wa Elimu kufanya msukumo wa kutambua changamoto ambazo hujitokeza kwenye sekta hiyo ya Elimu.

  


Maghembe amesema Halmashauri hiyo ina shule za Msingi 81 kati ya hizo shule 78 ni za Serikali na 03 ni shule zisizomilikiwa na Serikali huku shule za Sekondari zipo 22 kati ya hizo shule 17 ni za  Serikali na shule 05 za binafsi.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mkakati huo aliipongeza Halmashauri hiyo kwa kubuni mkakati huo ambao utasaidia wanafunzi kuwa na ufaulu mzuri.



Mkuu huyo ambaye amemuwakilisha Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais utumishi na Utawala bora amesema kuwa kama mkakati huo utazingatiwa kikamilifu Halmashauri hiyo itegemee kuwa na mabadiliko ya makubwa katika nyanja ya Elimu.

 

Aidha Ibuge licha ya kupongeza mkakati huo lakini bado ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kusimamia vema miradi ya  ujenzi wa madarasa yatokanayo na Uviko 19 ambayo sasa yanatumika na wanafunzi hao.



Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mennas Komba akitoa neno la shukurani kwa wadau mbalimbali wa Elimu alisema kuwa maagizo yote ambayo yamependekezwa kwenye mkakati huo kuwa yatafanyiwa kazi.



 Katika uzinduzi wa mkakati huo ambao uliyoambana na kaulimbiu ya Elimu bora inawezekana timiza wajibu wako ,huku shule zilizofanya vizuri kwenye taaluma zilipatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na vyeti.

        Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI