Header Ads Widget

HALMASHAURI YA CHAMWINO YAOMBWA KUITUPIA JICHO SEKTA YA ELIMU KATIKA BAJETI IJAYO

 




Klabu  za Wanafunzi  wa Shule za msingi na Sekondari  wameiomba Halmashauri ya ya Wilaya ya Chamwino  Mkoa wa Dodoma  kuitupia jicho sekta ya Elimu katika bajeti ijayo 2022/2023 ili kupunguza changamoto 10 zinazowakabili Wanafunzi hususani shule za msingi .



Miongoni mwa Changamoto hizo   ni pamoja na uhaba wa Matundu ya vyote, ukosefu wa vyumba vya faraga, uhaba wa Maji  mashuleni, ukosefu wa nyumba za Walimu, upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule za Sekondari, Na miundombinu mibovu kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.


Akiwasilisha mapendekezo  kwa uongozi wa Halmashauri  katika mkutano wa  wadau wa elimu uliondaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Actionaid Tanzania Mwenyekiti wa Club za Wanafunzi mashuleni  ambaye pia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa Wema Nollo  amesema‘’Unakuta shule moja inawanafunzi zaidi ya elfu moja na  inamatundu sita wasichana matatu na wavulana matatu, muda wa mapumziko ni dakika 20 wanaoenda kujisaidia ni wengi ,na msongamano ni mkubwa namuda muda wa vipindi unakuwa tayari umefika hii husababisha kuchelewa vipindi na wakati mwingine   inasababisha  kupata magonjwa  kama uti,’’


Akizungumzia changamoto ya umbali wa shule kwa wananfunzi  , Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri  Chamwino Editha Mabwe  ameiomba Serikali kuwajengea mabweni au shule karibu na vijiji ilikupunguza utoro na kukuza taaluma katika halmashauri hiyo.



‘’Shule nyingi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino zimejengwa mbali na makazi ya Kijiji kwa mfano Chilonwa, kuna wanafunzi wanatoka Mlimwa wanakuja kusoma shule ya sekondari Chilonwa,


‘’Kuna wanafunzi wanatoka Kijiji cha Chiwahele wanakuja kusoma Buigiri, hali ile inawasababishia wanafunzi kupata changamoto mbalimbali ikiwemo wasichana kubakwa,,’’amesema Mabwe.


 Akipokea mapendekezo hayo kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo  Edson Sweti amesema wameyapokea mapendekezo hayo  nawatayafanyia kazi kwa uharaka na kwawakati ili kutatua changamito hizo.


‘’Tutaa tushauriane na wenzetu hawa ili asilimia kubwa ya bajeti iende kwenye matundu ya vyoo, tunapotoka hapa tunaenda kuyafanyia kazi kwa kuwa changamoto hizi zimeanzia nyuma huko,’’amesema mwenyekiti huyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI