Header Ads Widget

CONGO (DRC) YAPITISHWA KUWA MWANACHAMA WA (EAC) RASMI




Teddy Kilanga _Arusha


Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki leo,Machi 29,2022 wameipitisha  Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama mpya wa  Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,(EAC) .



Kikao cha 19 cha wakuu wa nchi sita wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki,kilichofanyika leo Mach 29,2022,kwa njia ya mtandao , kikiongozwa  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais Uhuru Kenyatta  wa Kenya, DRC kuwa mwanachama mpya.  



Nchi saba wanachama wa EAC sasa ni Tanzania,Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na  DRC.



Wakuu hao walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame(Rwanda) Makamu wa Rais wa Burundi,Prosper Bazomba'nza, Waziri wa nchi ofisi ya Rais wa Sudan Kusini Dr Barnabas Benjamin na Rais wa DRC Felix Tshisekedi.



Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki amesema, DRC kujiunga na EAC una faida kubwa kiuchumi na kisiasa na kiulinzi ndani  ya  Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.




"Siku ya leo kwetu ni siku kuu ambayo ni ya heshima kwa jumuiya ya Afrika ya mashariki na wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki wameipitisha rasmi leo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kuwa Mwanachama wa EAC,"amesema Dkt.Mathuki.



Amesema ni furaha yao na wananchi wa EAC ikiwa kupiti Congo DRC kujiunga kutaongeza fursa za kiuchumi na kibiashara katika kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.



"Nchi hizi zikiondoa vikwazo mipakani katika kufanya biashara zitaongeza nafasi za ajira kwa wananchi kwani ndio lengo kuu wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya mashariki,"amesema Katibu Mtendaji wa EAC.



Katika nyanja ya kiuchumi, soko la jumuiya ya Afrika Mashariki, sasa linaongezeka kutoka milioni 190 na kuwa na watu zaidi ya takribani milioni 250 na kufanya kuwa miongoni mwa jumuiya kubwa za kikanda zenye watu wengi .



Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, tayari ilipitisha itifaki ya soko la pamoja, umoja wa forodha, sasa inaelekea katika itifaki ya sarafu moja na shirikisho la kisiasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI