Header Ads Widget

GEKUL AWAHIMIZA WASANII KUWA MABALOZI WA WIMBO WA TAIFA WA NCHI YA TANZANIA

 



Teddy Kilanga_ Arusha


Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo,Pauline Gekul  amewataka wasanii nchini kuwa mabalozi wazuri wa  wimbo wa Taifa, ili kuhakikisha hakuna mtu anayeweka vionjo vingine nje ya vilivyoasisiwa.


Akizungumza  wakati akifungua mkutano wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha,Gekul amesema kimsingi wimbo huo haupaswi kuchezewa kwa kuingiza vionjo au madogo mengine nje ya vilivyopo.


"Nawaomba nyie muwe mabalozi wa kulinda wimbo wetu huu ambao umeasisiwa na unaonyesha utaofa wetu,haifai kuongizwa madoido mengine  ambayo hayaleti utaifa wetu kama ulivyoasisiwa na wasisi wetu, unapaswa kubaki na usajili wake,"amesema.



Gekul amesema,fani ya uigizaji inamchango mkubwa kwa Taifa, kwani imekuwa na washiriki wazuri hasa wa kusimama mstari wa mbele kwenye kuhamasisha masuala mbalimbali ya Taifa.


"Kama wakati ule wa vita ya Nduli Idd Amini wasanii walishiriki kutunga nyimbo mbalimbali za kuhamasisha kumpigia adui huyo ili Taifa letu kibali salama,lakini katika vita dhidi ya Uviko-19 na Ukimwi pia tumeona,"alisema


Aidha,alisema kutokana na umuhimu huo Rais Samia Suluhu kaona umuhimu wa kufufua Mfuko wa  Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa kwa kuwapatia zaidi ya Sh.bilioni 1.4 ili kuwania kiuchumi waigizaji nchini.


Alisema kupitia fedha hizo wanaweza kukopa kwa riba nafuu na kuendeleza kazi zao huku wakichangia kukuza uchumi wa Taifa na wao binafsi.



Kuhusu ombi lao la kumuomba Rais Samia awe mgeni rasmi katika kongamano lao,alisema viongozi waandae ratiba rasmi na kufikisha wizarani ili ampigie Rais na anaamini anasikiliza ombi hilo.


Pia,aliomba  waigizaji kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri nchini ili nao wanufaike nayo. 


"Suala lenu mlilonipa hapa la  kupunguza kodi alisema Bodi ya Filamu ilikutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kupunguza kodi na tozo za wasanii na linafanyiwa kazi,"alisema



Aliwaasa kudumisha  umoja na upendo walionao ili chama chao kistawi na kufanya mambo makubwa zaidi ya kuinua Tania hiyo.


Gekul aliwaomba pia kuhakikisha wanapeleka chama hicho katika kila mkoa ambapo kwa sasa wapo  mikoa 22 kati ya 26 licha ya mikoa yote kuwa na wasanii.




Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) Salum Mchoma alisema chama hicho kinawachama hai 36,714  na kusisitiza kuwa wanamahitaji mbalimbali, kwani uigizaji ni rasilimali na kazi yao kubwa   kuikumbusha serikali na jamii kuwa sanaa ni muhimu katika uchumi wa nchi.



Alisema Tanzania inazaidi ya wasanii milioni 6 kati yao wasanii milioni 3 wanatokana na kazi za uagizaji lakini hawapo pamoja, hivyo vema serikali  kuwakusanya pamoja ili  kuwasaidia kutambulika.



Alisema sekta hiyo inamuingiliano wa aina mbalimbali na sekta mbalimbali hivyo alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kuwakumbuka na kuwakwamua kiuchumi kwa kuwapa Sh,bilioni 1.5 katika  mfuko wao, utakaowezesha kukopa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.



Pia waliomba kutambuliwa na Wizara ya Utumishi na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)kwani zinashikilia fedha kwaajili ya vijana,ajira na watu wenye ulemavu na kuomba chama hicho kitambuliwe ili wapate fedha za mikopo  ili waigizaji wapate maendelo na kujikwamua kiuchumi



"Tunaomba maafisa utamaduni watupokee vivyo hivyo ili tusikwame kimaendeleo pia tunaomba kupunguziwa na kuondolewa kodi na tozo ya kazi kwa wasanii ili  tusiwe na mzigo mkubwa wa gharama za kazi zetu,"alisema.




Alisema wanaishukuru Taasisi ya Haki Miliki Tanzania ( Cosota) kwakuwasaidia wasanii  pale wanapohitaji msaada wao.



Naye Msemaji wa Yanga na balozi wa kampuni ya GSM,Haji Manara alitoa rai kwa wasanii nchini kutumia  misingi ya Azimio la Arusha kwaajili ya kujikwamua kiuchumi kwani hali iliyopo hivi sasa kwa wasanii si ya kuridhisha kutokana na baadhi yao kuwa na majina makubwa lakini uhalisia wa kimaisha duni.



Alisisitiza umuhimu wa mkutano huo uwe chachu ya kujikwamua kiuchumi kwa wasanii kuwa na maslahi bora na kujikwamua kiukwasi kutokana na kazi zao.



Alisema GSM wawasaidia  wasanii kutoa vifaa mbalimbali kwaajili ya watu wenye uhitaji katika Hospitali ya Mount Meru ikiwemo kutoa fedha kwaajili ya kusaidia chama hicho cha wasanii kukua kiuchumi.



Mwenyekiti wa  chama cha waigizaji Mkoa wa Arusha,Fredrick Kephace  wamesema mkutano huo umewakutanisha wasanii waigizaji zaidi ya 150 kutoka mikoa 22 nchini.



"Lakini mikakati tuliyonayo kama Chama ni kuhakikisha wanawainua waigizaji mmoja mmoja pamoja na makundi hivyo wanatafuta wafadhiri na tayari wapo kwenya mazungumzo na baadhi ya wadau kuhakikisha  tunafanya filamu  ambazo zitatuinua na kufikia hatua za kimataifa,"alisema Mwenyekiti Kephace.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI