Wazazi/walezi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwa walinzi wa watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwa karibu nao ili waweze kuzingumza na watoto yale ambayo wanakutana nayo Mashuleni na sahemu mbalimbali na sio kuwaachia walimu peke Yao washughulike katika malezi.
Wito huo umetolewa na Immaculate Mworia mwezeshaji wa maswala ya ulinzi na usalama kwa watoto ,wakati alipokuwa akizungumza katika warsha iliyowakutanisha viongozi wa serikali za mitaa CGO pamoja na waalimu Iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Aidha amesema kuwa wazazi wametupa majukumu yao ya ulezi kwa waalimu jambo ambalo mwalimu hawezi kuzingumza na mtoto mda wote juu ya maswala ya Afya na mtoto.
"Tunanapozungunza afya ya mtoto tunazungumza maswala ya makuzi na balehe na mzazi anapokwepa hilo jukumu la malezi na kumuachia mwalimu ambaye kwake yeye ni taaluma yake ,anazungumza lakini ni kwa lugha ya kitaaluma ,lakini Ile lugha ya ndani inayotakiwa kutoka kwenye sauti ya baba na mama haitoki"Alisema Mworia.
Sambamba na hayo amesema kuwa kutokana na wazazi kutoongea na watoto wao imesababisha kuwepo kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto na wanashindwa kuwaeleza wazazi wao kwa sababu wazazi wamekuwa wakali kupita kiasi .
Ameendelea kusema kuwa wazazi wengine wenye kipato Cha juu wanakwepa malezi kwa kuwapeleka watoto shule za boarding na mwisho wa siku akiwa huko anayazoeya maisha ya kule na wale waliomzunguka mwisho wa siku anapokuwa mkubwa hawezi kumjua tabia yake kwa sababu yakutoshiriki katika malezi ya mtoto.
Kwa upande wake Belinda Eduard Afisa mradi wa wanawake na watoto katika shirika la Simba Footprint Foundation amesema kuwa lengo la mradi ni kuwapa elimu sahihi ya ukuaji na makuzi mabinti ambao mara nyingi wamekuwa hawaipati.
"Ukatili umekuwa ni mkubwa kwani umekuwa ukifanyika mpaka majumbani kwa wale wenye dhamana ya ulezi kwa watoto ,kwa hiyo tukaona tukiita hawa waalimu na hawa maafisa maendeleo ya jamii na viongozi wa mtaa tukashirikiana na Yale madawati ya jinsia , tunategemea kuwa na jukwaa la pamoja ambalo tutaweza kupashana habari na kuhakikisha kuwa jamii zile tunazohudumia watoto wanakuwa salama.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa shirika hilo Mkurugenzi wa Shirika la Footprint Foundation Charles Godfrey Masawe amesema kuwa lengo la shirika hilo ni kuwa sehemu ya kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii kwa kujaribu kugusa sehemu mbalimbali.
"Ukijaribu kuangalia kuna program sinahusu watoto, vijana , wanawake na Kuna jamii nzima kwa ujumla "Alisema Masawe.
Hata hivyo amesema lengo ni kutengeneza jukwaa ambalo litasimama kwa pamoja kuelezea maswala yanayohusu watoto na wanawake ambayo yamekuwa ni changamoto kwani Kumekuwepo na mgongano unaotokea kwenye haya magrupu mawili ya wanawake na watoto na kusema kuwa wasipopaza sauti jamii ambayo haijali na haieshimu haki za wanawake na watoto.
0 Comments