Header Ads Widget

WANANCHI WAGUSWA NA UTENDAJI WA MWENYEKITI CCM MARA WAFUNGUKA MAMBO MAZITO



NA MWANDISHI WETU,MARA


WANANCHI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara wamesema muda ukifika wapo tayari kwa gharama yoyote kumchukulia fomu ya kuwania nafasi ya uwenyekiti Mwenyekiti wa CCM mkoa,Samuel Kiboye (Namba Tatu) kwa sababu ni kati ya viongozi walioonesha uthubutu katika kukisimamia chama.


Sambamba na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa ukaribu na kusimama imara kwa kumtetea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.


"Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa nchini inayohitaji viongozi hodari, shupavu na majasiri katika kusimamia, kufuatilia shughuli za chama na miradi ya maendeleo. Ukiwa legelege, utajikuta wenzako wanatumia nafasi zao kujineemesha huku maendeleo ya chama na miradi ya maendeleo ikisuasua. Kwa hilo, nikiri wazi kuwa,Namba Tatu (Samuel Kiboye) kwa kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kulidhibiti.


"Yule kiongozi (Samuel Kiboye), kwanza ni mtu jasiri, asiyeogopa kusema ukweli kwa ajili ya kuwaonea aibu wajanja wajanja na tumeona kwa namna ambavyo heshima ya chama imerejea, kufanikisha tu, maadhimisho ya miaka 45 ya chama hapa mkoani Mara ni moja wapo ya mafanikio makubwa kwake, miaka ya nyuma hilo lisingefanikiwa kwa ufanisi ulioonekana.


"Kwa msingi huo, muda ukifika tupo tayari kwa gharama zozote kumchukulia ndugu Namba Tatu fomu ili aendelee kukisimamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara na akaendelee kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi katika halmashauri za wilaya ili wananchi tuweze kunufaika na maendeleo yanayoletwa na Serikali ya Awamu ya Sita,"amesema Charles Mariba mkazi wa Musoma Vijijini.


Wakati huo huo, wamewmtaka Mwenyekiti huyo kuendelea na misimamo yake ya kuendelea kuyaeleza kwa Watanzania mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwani amekuwa kiongozi wa kipekee katika chama ambaye huwa anajitokeza hadharani kuelezea mafanikio mbalimbali ya Serikali na miradi inayotekelezwa kuanzia mijini na vijijini.


"Pia mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kutupa hamasa ya kuliombea Taifa na viongozi wake chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, na hakika wito huo umekuwa ukipokelewa vizuri sana, nahisi Namba Tatu ni miongoni mwa viongozi wenye hofu kubwa ya Mungu, na ndiyo viongozi tunaowahitaji katika chama na Serikali ili hofu ya Mungu itumike kulineemesha Taifa na jamii zetu na siyo wachache kujinufaisha kupitia madaraka,"amesema Ester Julius mkazi wa Musoma Mjini.


Wameongeza kuwa, Kiboye amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kukifanya chama kuwa imara ikiwemo kuyadhibiti makundi ambayo mara nyingi yalikuwa kikwazo katika mustakabali wa chama hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI