NA WILLIUM PAUL, HAI.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kimewahimiza viongozi na wanachama wake kuendelea kudumisha amani ,upendo na ushirikiano ili kuweza kutekeleza na kutimiza matarajio ya wananchi ya kupata maendeleo kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kimewahimiza viongozi na wanachama wake kuendelea kudumisha amani ,upendo na ushirikiano ili kuweza kutekeleza na kutimiza matarajio ya wananchi ya kupata maendeleo kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai, Waguba Maganda wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyi kiwilaya kwenye uwanja wa Bomani,ambapo licha ya kusisitiza mshikamano pamoja na mabo mengine ,amewataka wenye sifa za uongozi chukua fomu za kugombea katika chaguzi zijazo ndani ya Chama.
Maganda alisema kuwa, mwaka huu chama hicho kinauchaguzi ndani ya chama hivyo ni jukumu la kila mwanachama mwenye sifa kujitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
"Wanaccm tunapaswa kuendelea kudumisha upendo, amani na ushirikiano mkubwa kwa viongozi wetu wa chama na Serikali tuwaunge mkono ili kuhakikisha tunawatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi ambao ndio waliotuchagua" alisema Maganda.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kamati ya siasa wilaya haitakuwa tayari kupokea malalamiko ya wanachama kunyimwa kuchukua fomu na kuwataka viongozi wa chama kuanzia kata kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba huku akiwaonya kutobeba wagombea.
Amewataka kuhakikisha uchaguzi unaoenda kufanyika ndani ya chama unaenda kuwa huru na haki ili kuwapata viongozi bora ambao watachaguliwa na wanachama wenyewe na sio wao kuchaguliwa viongozi.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa, wilaya ya Hai kwa sasa imeanza kubadilika kwa kupata maendeleo makubwa kutokana na kupata mtu sahihi wa kuisemea na kuyasemea matatizo ya wananchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo Saashisha Mafue.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai, Edmund Lutaraka alisema wanajivunia mambo mengi ya maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita na kuwataka viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi kwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Lutaraka alisema kuwa, wilaya ya Hai ilikuwa na upungufu wa madarasa ambapo Rais Samia Suluhu alitambua changamoto hiyo na kuiletea wilaya hiyo milioni 860 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 43 hali ambayo imepelekea kumaliza tatizo hilo.
Alisema kuwa, lipo tatizo la maji katika baadhi ya maeneo ya Hai ambapo serikali imeshaleta Bilioni 3.5 kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo ambapo kwa sasa mkandarasi yupo saiti.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Hai, Juma Irando alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa jinsi anvyotoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo na kuahidi kuwa miradi yote itakayokuwa ikijengwa ndani ya wilaya hiyo itakuwa bora huku dhamani ya fedha ikionekana.
Mwisho.
0 Comments