Header Ads Widget

WAKULIMA WAPEWA ELIMU YA JINSI YA KUDHIBITI WADUDU WAHARIBIFU

 


Na Rehema Abraham


Imeelezwa kuwa wakulima walio wengi hawatambui  namna ya kudhibiti  wadudu waharibifu kwa njia iliyosalama jambo ambalo limesasababisha wakulima kutumia kemikali za viwandani zinazosababisha uharibifu wa mazingira.



 Aidha wadau wa kilimo hai wanaendelea kutoa elimu  kwa wakulima juu ya jinsi ya kudhibiti wadudu hao kwa njia za asili ya kutumia mimea ambayo haina madhara kwa mkulima na mlaji. 


Akizungumza katika mafunzo hayo Doctor.Angela Gerald mkindi ambaye ni  mhadhiri na mtafiti kutoka chuo kikuu Cha sayansi Cha Nelson Mandela  kilichopo Arusha Amesema kuwa katika mafunzo hayo wanaangalia namna ya kutunza Ekolojia mazingira yaliyopo katika maeneo ya kilimo ili kuweza kusaidia katika kupunguza au kumaliza kabisa madhara ya wadudu waharibifu .



"Tunajua kabisa ardhi na mazingira yetu yanahitaji uwiano flani ambao unasaidia katika njia zake za asili za kudhibiti na kupunguza athari za waadudu waaribifu ,tuna mifano mingi sana ya majanga ambao wadudu wanakuwa wengi na mazao yanaisha kwa wingi lakini tukiangalia vizuri sana kwa nyuma na kwa kina zaidi ni kwa sababu mazingira yameharibika , Ekolojia haina Ile balance yake iliyokuwepo mpaka Sasa tunaenda kulazimika kutumia viuwatilifu vya viwandani ambavyo vimeonekana kwa uthibitisho kwamba vina madhara kwa binadamu na kwa wadudu wenyewe"Alisema Mkindi.



Sambamba na hayo amesema kuwa ni vizuri wakulima na watafiti wakakaa pamoja kujadili kinachoendelea ni nini,na kilichoharibika ni nini na mbinu za kutumia ili kunusuru kilimo.


"Nimefanya tafiti nyingi sana katika miti na  mimea mbalimbali ambazo zinaweza kudhibiti wadudu waharibifu na hizi ni salama zaidi kwamba haina Ile wingi wa ubaya wa kuharibu mazingira"Alisema.


Katika hatua nyingine amesema kuwa mfano ya miti hiyo ni Kama mwaribaini ,pilipili, tangawizi ,karafuu na miti mingine ambayo hailiwi na wanadamu lakini haina madhara makubwa kwa mwanadamu.



Hata hivyo Amesema mafunzo hayo ni matokeo ya kazi ambayo inaendelea kwa nchi mbili ambayo ni Malawi na Tanzania kwa ufadhili wa watu wa marekani ambao ni magnite foundation, pamoja na washirika kutoka Green which,na royal botanical garden .


Nao wakulima walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Athumani Ramadhani kutoka wilaya ya same amesema kuwa kwa sasa wanalima kilimo kinachotumia kilimo hai kwani hapo nyuma walikuwa wanatumia madawa ya viwandani ambayo Ina madhara kwa afya .


Amesema kuwa kwa jinsi wavyopewa mafunzo hayo ya mwendelezo wa madawa ya asili itakuwa faraja kwao na wengine wanaowauzia mazao 


Hata hivyo Amesema kuwa Kuna faida katika kilimo hai kwani hakina madhara kwa mkulima na mlaji .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI