Kikongwe (100) Jane Kibondo mkazi wa kijiji cha Kwambe kata ya Dumila amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga kwa kumsaidia kurejeshewa Shamba lake zaidi ya hekari 6 alizodhurumiwa na aliyekua mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Mkunda Yohana .
Hivi karibu Mkuu wa. Wilaya ya Kilosa Alahj Majid Mwanga alipokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa mjukuu wa Bibi huyo ukielezwa namna walivyodhurumiwa Shamba Hilo na Bwana Mkunda Yohana kwa Kuuza kwa watu mbalimbali bila ridhaa yao
Baada ya kupata ujumbe mfupi kutoka kwa mjuku wa bibi huyo akalazimika kufika katika eneo Hilo ili kufahamu ukweli wa tukio hilo.
Baada ya kufika katika eneo hilo Kikongwe huyo anadai kuwa Miaka kadhaa iliyopita walimpatia Bwana Mkunda eneo hilo kwa lengo la kuishi lakini badae aligeuka na kuanza Kuuza eneo lote huku akidai kuwa eneo ni lake na akikana ajapewa na kikongwe huyo
Baada ya kupata malalamiko hayo DC Mwanga analazimika kutoa maagizo kwa serikali ya kijiji ili kumsaidia arejeshewe eneo hilo bila masharti kwani eneo Hilo NI mali yake kwani mwenyekiti huyo mstafu alipewa kwa muda.
Baada ya maagizo hayo Viongozi wa vijijini wanashirikiana kwa pamoja na kufanikiwa kumrejeshea kikongwe Shamba lake Jambo ambalo kikongwe huyo amemshukuru Dc Mwanga kwa msimamo wake wa kutetea haki za wananchi wanyonge
DC Mwanga amekua na utaratibu wa kutoa namba ya Simu kwa wananchi wote wa Wilaya hiyo katika mikutano yake ya hadhara ili iwe fursa kwa wananchi wanaoshindwa kufika katika ofsi yake kutoa malalamiko badala yake malalamiko yao wanafikisha kwa njia ya SMS au kupiga Simu ili changamoto zao zitatuliwe ambapo zoezi Hilo limeonekana kuzaa matunda Kila siku
MWISHO
0 Comments