Header Ads Widget

USIKU WA KWANZA WA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2022 WANOGA ZANZIBAR

Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara, Mahmoud Yusuf

TAMASHA kubwa la muziki la Kimataifa la Sauti za Busara 2022  limeanza rasmi jioni ya February 11,2022 huku bendi na Wasanii wakinogesha kwa midundo ya muziki wa Kiafrika kwenye jukwaa kubwa ndani ya Mambo Club, Unguja Visiwani hapa, Zanzibar.Mwandishi Andrew Chale, MDTV Zanzibar

Tamaha hilo lenye kauli mbiu ya Paza Sauti; Amplifying Women’s Voices, limewahusisha wanawake zaidi, ambao mwaka huu wapo zaidi ya sita, mbali ya wale walio kwenye bendi yenye mchanganyiko. 



Shoo hiyo ya kwanza katika jukwaa hilo la Mambo Club, limefunguliwa na msanii Upendo Manase kutoka Tanzania Bara, wakifuatiwa na wasanii wengine; Evans Pfumela Mapfumo [Zimbabwe], Nadi Ikhan Safaa [Zanzibar].


Pia wasanii wengine ni; Fanie Fayar [Congo],  Nomfusi [Afrika Kusini], Lakini pia wasanii wengine Ben Pol aliweza kushika vilivyo jukwaa kwa nyimbo zake mpya na za zamani huku bendi iliyofunga usiku wa siku ya kwanza yab Zan Ubuntu kutoka  visiwani hapa, Zanzibar


Wasanii hao kwa nyakati tofauti wameweza kukonga nyoyo fans waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo la siku ya kwanza.

Bendi ya inayopiga muziki wa taarab Asilia ambapo wameweza kunogesha kwa aina hiyo ya muziki.




Awali akizungumza katika neno la ufunguzi wa tamasha, Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmud alishukuru watu waliojitokeza kufurahia muziki mzuri wenye ladha tofauti ya kiafrika, ambapo amewataka kuendelea kuwaunga mkono kwa siku zote za uwepo wa tamasha.


Amewataka wadau kufurahia fursa za tamasha hilo zikiwemo za kiuchumi na biashara kutoka Ulimwenguni kote wanaofika Visiwani hapa.


‘’Wageni mbalimbali wanapata kufurahia muziki mzuri lakini pia wanapata fursa za kutalii na kuona uzuri wa Zanzibar.


Aidha, Mahmoud Yusuf alisema kuwa, kuna hati hati ya kufanyika ama kutofanyika kwa msimu wa 20.


‘’Safari hii tunafikia mwisho wa uwepo wa tamasha kwani tutashindwa kuendelea msimu ujao kutokana na kukosa fedha za kuendesha tamasha.



Kiasi cha fedha kidogo ikiwemo kiingilio chenu ndio tunaendeshea tamasha la msimu huu ikiwa kurejesha malipo mbalimbali yanayotumika sasa hapa kwa siku zote tatu... tunaendekea kuiomba Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia 


Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.’’ Alisema Mahmoud Yusuf.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI