Header Ads Widget

DKT MIPANGO AZINDUA SERA MPYA YA TAIFA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amezindua Sera mpya ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 na mpango mkakati wake huku akimtaka Waziri Jafo kuunda timu itakayokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,kwakushirikiana na Jiji la Dodoma  na Wakala wa misitu nchini TFS na TAMISEMI kuandaa Mpango Mkakati wakukijanisha Miji natimu hiyo iwe inampa taarifa ya utekelezaji wake Kila baada ya miezi mitatu.mwandushi Hamida Ramadhani MDTV  Dodoma


Akiongea katika uzinduzi huo Dkt Mpango amesema suala la Uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya 6  yanaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  huku akieeleza taarifa ya mwisho ya hali ya mazingira nchini ya mwaka 2019 ilionesha wazi kunamapungufu mengi kuhusu namna inavyotekeleza sera na sheria za uhifadhi zinazohusu mazingira



Amesema kuwa, Kumekuwa na ongezeko kubwa la uharibifu wa ardhi kutokana na shuguli mbalimbali ikiwemo Ufugaji kilimo kisichokuwa na mpangilio na ukataji wa miti hovyo kiwango cha uharibifu wa ardhi kimeongezeka kutoka asimia 42 mwaka 1980 hadi asilimia 50 mwaka  2012 na asilimia 63 mwaka 2018.


" Kama Taifa hatuna budi kuimarisha mipango mikakati ya utekekezaji ambao unajumuisha ufuatiliaji usimamizi dhabiti na kufanya tathimini ya mara kwa mara huku,"amesema Dkt Mpango 


Amesema, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira inayo dhamana ya kuhakikisha sera hiyo inatekekezeka kikamilifu ikiwa ni pamoja ya kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani na yenye mazingira safi. 


" Tumekuwa na mipango mingi lakini utekelezaji wake umekuwa bado hauridhishi tusitekeleze agenda hii kwa uhai wa taifa letu muhimu kwa mazoea tusiishie kwenye matamshi ya kisera na kauli mbiu tu ni lazima kuanzia sasa tufanye kazi ya ziada na tujiwekee viashiria vinavyopima na vitakavyonyesha nikweli tumefanya kazi katika taifa letu.


Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema mkoa wa  Dodoma unaonekana ni mkoa kame lakini ukweli ni kwamba mkoa huo sio kame kama inavyofahamika kwani mkoa huo una udongo mzuri na wenye rutuba ambapo amesema udongo wake ukipata maji kidogo unastawisha kila aina ya mmea.


"Tukio hili ni endelevu na sio tukio la Dodoma pekee bali ni zoezi la nchi nzima kwani tunayo sababu ya kupanda miti ya aina yote ya matunda mbao dawa na hata ya viungo tulishuhudia tukikabiliwa na ukame katika miezi ya nyuma hivyo niwaombe kila mmoja asimamie hili kikamilifu,"amesema


Awali akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasimi Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Sulemani Jafo amesema uzinduzi wa sera hiyo inakwenda litekeleze masuala mbalimbali  ambayo yatakwenda kukomboa taifa la Tanzania. 


Amesema maelekezo yake ya kila siku kutaka  kutunza na kulinda mazingira muda wote na ndio maana katika vipindi mbalimbali na serikali imeelekeza kila Halmashauri kupanda miti Milioni 1.5 kwa Halmashauri zote 184 lengo ni kupata miti Milioni 276 kwa mwaka Zaidi ya miti 141,000 imepandwa katika wiki hiyo huku akieleza lengo nikupanda miti Milioni 14.5 kulingana na idadi ya wanafunzi mashuleni katika kipindi hiki cha mvua.


Awali Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji na Mazingira ,David Kihenzile amesema mefurahia kubadilishwa kwa Sera ya Mazingira ambayo imedumu muda mrefu huku akitoa rai kwa Serikali kufanya mchakato kwenda kwenye Sheria na kanuni.


Hata hivyo uzinduzi huo umeenda sambamba na kilele Cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira ambayo yalianza rasmi February 7 Mwaka huu ambayo iliambatana na upandaji miti pamoja na usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Dodoma na yamehitimishwa na kaulimbiu isemayo 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI