Header Ads Widget

SERIKALI YAJIPANGA KUKUSANYA BIL.650, MAGARI 40 YAZINDULIWA

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Waziri wa MADINI Dkt  Dotto Biteko amewataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha magari waliyokabidhiwa yanatunzwa na kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuhakikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 650 kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 linafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.


Kauli hiyo, ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akikadbidi na kuzindua  magari saba kati ya magari 40 yanayotarajiwa kutolewa na Serikali kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.


Amesema kuwa, magari hayo yatatumika kama kichocheo cha ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini, Ili kuleta matokeo chanya kwa Serikali na wachimbaji.


Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kununua vifaa vingine kama vile mashine za kupima madini kwenye masoko ya madini na kusimamia kwa karibu shughuli za madini ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yake stahiki.


Katika hatua nyingine akizungumzia mikakati iliyowekwa na Wizara ya Madini kwenye udhibiti wa utoroshaji wa madini, amesema kuwa mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza maafisa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.


Aidha, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa Serikali haitamuonea huruma mtu yeyote ayakayebainika anatorosha madini.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula amesema kuwa magari hayo yatarahisisha kwa kiasi kikubwa utendaji kazi kwa kufika maeneo yasiyofikika kirahisi. 


Aidha, ameipongeza Serikali kupitia Wizara kununua magari hayo yatakwenda kusaidia katika uzalishaji wa mapato makubwa kwa Serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI