Header Ads Widget

MSIMU WA 20 WA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2023 KUFANYIKA-SERIKALI

 


Na Andrew Chale, Zanzibar. 


SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewahakikishia wadau wa burudani kuwa tamasha kubwa la muziki na la Kimataifa la Sauti za Busara msimu wa 20, litafanyika.



Waziri Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa Februari 13,2022, wakati wa kufunga kwa tamasha la msimu wa 19 mbele ya umati mkubwa wa wadau wa burudani.


"Niwapongeze sana Sauti za Busara kwa kazi kubwa na nzuri kwa maandalizi haya, Sisi kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunawaunga mkono sana.


Tumepata taarifa kuwa kuna 'kaugumu' kidogo  katika maandalizi ya tamasha linalokuja, Kama Serikali tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba linaenda kufanyika." Alisema Waziri Mchengerwa  huku akipata shangwe kwa wadau na wapenzi wa burudani waliojitokeza kwenye tamasha hilo.


Ambapo alirejea tena kwa msisitizo kwa wadau hao:

"...Sauti za Busara linaenda kufanyika Serikali inawahakikishia litafanyika.".


Aidha, ametumia wasaha huo kuwakaribisha wageni mbalimbali kwenye matamasha mengine makubwa yaliyoanzishwa yakiwemo yale ya Serikali na wadau binafsi.


"Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Samia Suluhu Hassan amekwisha aanzisha matamash kadhaa, tutakuwa na Serengeti Festival mwezi Machi 12,2022 Mjini  Dodoma, tunawakaribisha sana Dodoma watanzania wote na wageni kwa ujumla.


"Pia mwezi wa Oktoba kule Bagamoyo, karibuni sana tusheherekee kwa pamoja" alisema Waziri Mchengerwa. 


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions waandaji wa tamasha hilo, Mhe. Simai Mohammed Simai (MB) Amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kutoa kauli hiyo ya Serikali ambayo ni sikivu


Ambapo alishukuru kwa niaba ya wajumbe wote Busara Promotions ambapo limekuwa chachu ya ukuaji wa uchumi katika kupitia Utalii visiwani hapa.


Serikali inaandaa matamasha hayo makubwa ya kihistoria ambayo yataonesha utamaduni wa kitanzania, wageni mbalimbali wanakaribishwa kushuhudia matukio hayo ya kimataifa kwani yanakwenda kuionyesha dunia utajiri wa utamaduni na vivutio vya utalii duniani.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS