Header Ads Widget

JIJI LA DODOMA LAWEKA REKODI YA JUU YA WA MIKOPO YA MAGARI,BAJAJI,GUTA NA BODABODA KWA VIKUNDI

 



HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imekabidhi vifaa mbalimbali kwa vikundi vya Ujasiriamali ikiwa ni pamoja na lori aina ya fuso tani saba kwa ajili ya kubebea mchanga na matofali, ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo yanatakiwa kurejeshwa kama mkopo kwa Vijana, Wanawake, na Watu Wenye Ulemavu.


Akikabidhi mikopo hiyo leo Februari 3, 2022, mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesema kuwa mikopo hiyo ni kwa ajili ya shughuli za viwanda,Guta 1,Lori moja la kubebea tofari na mchanga,fuso tani saba na mikopo kwa ajili ya biashara  ndogondogo, mikopo ya kilimo,mikopo ya mifugo na mikopo kwa ajili ya mama lishe na baba lishe.


Shekimweri alisema kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha halmashauri ya Jiji la Dodoma imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi 817,400,000 kwa vikundi 78 vilivyokabidhiwa hundi leo.


"Mikopo hii itumike katika kuwaletea maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja,jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla kwa kutimiza niya ya serikali ya kukuza uchumi wa mtu na uchumi wa vitu" alieleza Shekimweri.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru alisema kuwa, katika kutekeleza sera ya kutoa asilimia kumi katika makundi ya vijana,akina mama na makundi maalumu halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kipindi cha mwaka wa fedha imetoa jumla ya mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.87.


"Vile vile taarifa inaonesha kwamba shilingi 3,981,070,933.62 tu ndizo zimerejeshwa ambapo ni sawa na asilimia 44.9 ya kiasi kilichotolewa cha mikopo iliyotolewa"amesema.


Mkurugenzi Mafuru amesema kuwa katika mikopo iliyotolewa leo kwa upande wa vikundi 46 vya wanawake wamepata sh.395,000,000, vikundi 23 vya vijana wamepata sh.364,000,000 na vikundi 19 vya watu wenye ulemavu wamepata sh.58,400,000 na kufanya jumla ya vikundi 78 kupata jumla ya fedha sh.817,400,000.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde pamoja na  Naibu Meya wa Jiji la Dodoma *Mh.Emmanuel Chibago* wamewataka wanavikundi wote wanaonufaika na mikopo hiyo kuitumia kwa lengo lililokusudiwa huku wakiimwagia sifa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutekelezwa kwa kiwango kikubwa takwa hilo la kisheria la kutoa asilimia kumi ya  mapato ya ndani kwa makundi hayo.


Akitoa ushuhuda katika hafla hiyo, mwenyekiti wa kikundi cha Ilumbo Group ambacho kilishanufaika na utaratibu huo Bi.Monica Masado alisema kikundi hicho kimekuwa wanufaika wakuu wa mikopo kutoka katika halmashuri ya Jiji la Dodoma.



Monica alisema kuwa mikopo hiyo ambayo inatolewa na halmashauri ya Jiji imeweza kuinua maisha ya watu pamoja familia zao.


Hata hivyo amesema wakopaji wanaokopa wanatakiwa kuhakikisha wanakopa na kurejesha kwa wakati.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI