Wananchi Wa Kijiji Cha Chabima kata ya Masanze Wilaya ya Kilosa Mkoa Morogoro wameshindwa kificha hisia zao na kupaza sauti kwa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo baada ya kumuona MKUU wa Wilaya hiyo Alhaj Majd Mwanga nakusema kuwa huyo ndo mkuu Wa Kwanza wa Wilaya kufika katika Kijiji hicho tangu Miaka 20 iliyopita.
Mjumbe wa Kijiji hicho Cha Chabima Daniel Kasimu Anasema tangu ameshika nafasi hiyi ni zaidi ya Miaka 20 hajawahi kuona mkuu wa wilaya Wala mkurugenzi kufika na kuwasilikiza kero zao hivyo kitendo Cha DC Mwanga kufika Kijiji hapo wanaona ni faraja kuwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan upo imara na unawajali wananchi
Kassimu anasema Kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo barabara na sehemu za kupatia huduma za afya hivyo kufika kwa DC wanaona ni fursa ya kupaza sauti ili kero zao ziweze kutatuliwa.
Kassimu anaongeza kwa kusema kuwa wanamshuru Rias wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Milioni Mia 5 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya katika Kata ya Masanze
"Mheshimiwa DC naomba tufikishie Salam zetu kwa Mheshimiwa Rais Samia kwa kutuletea kiongozi imara na muwajibikaji hakika wew unatufaa hajafanya makosa " Daniel Kassimu mkazi Chabima.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga amesema lengo la serikali ya awamu ya Sita ni kuwasaidia wananchi hivyo atahakikisha kituo hicho Cha Afya kinakamilika kwa wakati.
Pamoja na hayo DC Mwanga akatumia nafasi hiyo kuhamasisha wananchi kuchanja CHANJO ya UVICO 19 pamoja na kunianda na Sensa mwezi agosti Mwaka huu.
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilosa ilitembelea Kijiji hicho kufuatilia mradi wa mkaa Endelevu uliopo chini ya TFCG lengo kufahamu miradi ya maendeleo inavyowanufaisha wananchi
0 Comments