Adeladius Makwega-DODOMA
Katika matini iliyotangulia nilieleza namna utani wa WAPARE ulivyotokea huku nikitaja hata jina la kabila hili la asili na namna jina jipya lilivyotokea.
Ndugu S. Mesaki katika utafiti wake juu ya Utani wa Wapare anasema kuwa kama MBANGA akifariki ambaye ni ukoo watawala mwenye wajibu wa kuchukua mifupa na fuvu la marehemu na kulipeleka katika msitu wa WACHONVU.
Mchonvu akifanya kazi hiyo kama maziko ndiyo kusema wao walikuwa na utaratibu kuwa mwili huo ulikuwa ukihifadhi hadi uharibike alafu mifupa ndiyo inayopelekwa msituni kama maziko.
“MCHONVU huyu akishamaliza kazi hiyo alikuwa akilipwa mbuzi au fahari ( dume kubwa la ng’ombe) wanyam hao walitolewa kama ujira kwa kazi hiyo. Mara akishalipwa huwa anasema maeneo kuwa mbona hafi MBANGA mwinngine ili apate dume la ng’ombe lingine? ”
Pia panapotokea msiba mtani hupewa kazi ya kugawa mali za marehemu kwani yeye huwa hana aibu na anaweza kusema maneno kama haya.
“Ghuna icho ambu nich meirihirwe akinafwe.”
Akimaanisha kuwa chukua hiyo kwa kuwa una furaha kwa kuwa amefaki. Maneno hayo yakiambatana na mgao wa nguo au mali zingine za marehemu.
Mtani hawezi kuishia hapo bali anaweza kusema maneno haya:
“Mie senafwa se nani erundie.”
Hapa akimaanisha kuwa yeye hawezi kufa kama alivyokufa mtani wake, anafanya hivyo hiyo akijilinganisha na kifo cha marehemu ambaye anatoka kwa watani wake.
“Ula mghoma wafwa.”
Akimaanisha yule ng’ombe mkongwe amefariki akimlinganisha marehemu ambaye alikuwa mzee na ng’ombe.
Pia mtani anaweza kwenda mbali kabisa kwa kusema:
“Kama wala kiteta.”
Hapa akimaanisha kuwa kama ndugu wa marehemu wameshamla nyama marehemu huyo.
Utani unaonekana katika mazishi ambapo kaburi likiwa limeshachimbwa na mwili wa marehemu upo unataka kuzikwa basi mtani anaweza kuingia ndani ya kaburi na kusema hatoki hadi apewe mbuzi. Hilo kweli hufanyika na mtani hupewa mbuzi alafu mazishi hufanyika.
Wapare ni kabila lililokuwa linafanya tohara kwa wavulana na wasichana kabla ya sheria kukataza tohara ya wasichana. Wakati shughuli hiyo kulikuwa na aina ya utani ambayo ilikuwa inafanywa hasa wale wazazi waliotahiri watoto wao awali na wale wanaofanyiwa tohara kwa siku hiyo.
Utani huo ulikuwa unafanywa kwa nia kama ya kuwapongeza kwa watoto hao kwa kufikia hatua hiyo ya utu uzima na kueleza umuhimu wa shughuli hiyo kwa kabila hilo.
Utani huo ulikuwa ni wa wazazi kwa wazazi tu. Kwa wale waliofanyiwa tohara ilikuwa ni pongezi.Utani katika shughuli hiyo uliendana na nyimbo huku pongezi zikitolewa.
“Idhihira, waehija, eee, wenyongie ukabanda, eee…iki nimuenda mbora wako…”
Wakimaanisha kuwa ulikuwa mwembamba lakini sasa umekuwa mnene.Maana yake baada ya kufanyiwa tohara hiyo sasa umekuwa mkubwa na umenawili.
Mwanakwetu naomba niishie hapo kwa leo.
Je kipi kitafuta ?
Subiri matini ijayo.
makwadeladius@gmai.com
0717649257
0 Comments