Adeladius Makwega DODOMA.
Katika sehemu ya kwanza ya matini juu ya Wajita nilizungumzia koo tano za Wajita, sasa ninakodolea macho yangu yote katika utani wa Wajita na Wabauluguru.
Utani wa kwanza wa Wajita unapatikana katika ya ukoo wa Wabalinga na Wabegunda, koo hizi mbili za Wajita, hawa wanaishi katika maeneo jirani, kuna wakati ikidaiwa kuwa Wabalinga na Wabegunda walikuwa wakijenga nyumba pamoja. Wakiwa katika kazi hiyo kiliandaliwa chakula cha kula ambacho kilikuwa nyama.
Wabalinga walikuwa hawali nyama ambao imepikwa tayari, Wabegunda walikuwa nyama katika kazi hiyo ya ujenzi. Wabalinga wakawapa Wabeganda samaki ambaye alikuwa na simu na wao wakafa, tukio hilo lilisababisha watu wengi kufa na miili yao ikaelea katika ziwa. Kukaibuka vita vikubwa mno na hapo ndipo Wabalinga wakafukuzwa katika eneo la Buongo.
Baada ya tukio hilo ukaibuka utani wa koo hizo mbili. Huku ikiaminika kuwa Wabegamba ni wawindaji. Kuna siku walisababisha kifo cha babu yao wakidhani ni kiboko, huku jambo hilo likisababisha wao kutaniwa kwa umelo wa nyama hadi wakamuua babu yao.
Utani unaonekana katika koo za Wabagunda ambao ni wawindaji zaidi ya koo zote za Wajita. Jina lao linatokokana na neno Kugunda ikimanisha kuwinda, wakiamini koo zingine zote za wajita hazijui namna ya kutumia mkuki na upinde na koo hizo ni za wavuvi. Wabagunda wanatambua kuwa kazi kubwa ya koo zingine ni uvuvi. Wabagumba wanawatania koo zingine kuwa ni waoga wanaoogopa wanyama kama simba na chui.
Japokuwa Wabagunda wanajinasibu kuwa na silaha zote hizo lakini koo zingine za Wajita zinawadhalau ndugu hawa kuwa hawana chifu, hawana mtawala na mambo yao yanajiendea tu. Kwa mfano ukoo wa Wabegamba ni mabingwa wa kusema hilo wa Wabagunda.
Pia utani unaonekana baina ya Wajita na Wabaluguru, Wabaluguru ni watu wanaoishi mashariki ya Majita. Huko wapo Wakuria, Wazanaki na Wangororeme. Wabaluguru kwa desturi wanatazamwa na Wajita kama wezi wa ngombe. Panapotokea uvamizi huo ambapo wanatumia mikuki mishale na marungu. Wajita ili kuwa salama basi hukimbili Ziwani Victoria kwa kutumia mitumbwi.
Wanaporudi wanakutana na makazi yao yakiwa tupu huku mifugo yote imeibwa. Ikiaminika kuwa Wajita hawana tabia ya kurudisha mapigo baada ya kufanyiwa ubaya.
Tabia hiyo ya wizi wa mifugo ya Wajita iliifanya jamii ya Wajita kukataa katakata kuona na Wabaluguru kwani kwa kufanya hivyo Wajita waliamini kuwa wanamkaribisha mwizi jirani ili aje kuiba zaidi mifugo yao.
Wabaluguru huwa ni walaji wakubwa wa uyoga, jambo hilo linawafaya Wajita kuwadhalau zaidi wa Wabaluguru kwani uyoga huo Wajita huita “Bitebe bya Nyamkoro” wakimaanisha kuwa uyoga ni kiti cha wavivu..
Utani mwingine wanaoufanya Wajita kwa Wabaluguru ni juu ya usafi. Wajita wanadai kuwa Wabaluguru ni wachafu kwani wanaweza kukaa miaka na miaka bila ya kuoga. Huku Wabaluguru wenyewe wanadai kuwa Wajita kazi yao kubwa ni kushinda katika maji kama samaiki, wakioga kila mara. Wabaluguru wanasema kuwa mikono ya Wajita inamomonyoka kwa kushika maji kila mara.
Mwanamke wa Kibaluguru anatazamwa kuwa hana desturi ya kuoga kila mara kama ilivyo kwa wanawake wa Kijita. Huku ikiaminika kuwa wanawake wa kijita (Hashakumu si matusi) wamekuwa na destruri ya kuosha tupu (uke) zao kila mara hiyo ikitazamwa na Wabaluguru kuwa ni ishara ya ukahaba.
Kwa desturi Wabaluguru huwa wanafanya tohara ya wanawake lakini Wajita hilo huwa halifanyiki na kutokufanya kwao tohara kwa Wajita Wabaluguru wakiwatazama wanawake wa Kijita kama makahaba.
Japokuwa sasa inawezekana kuwa wizi wa ng’ombe haufanyiki sana kutokana na kuwepo kwa vyombo imara vya ulinzi na usalama na sheria kadhaa za kukataza ukeketaji wa wanawake lakini mitazamo hiyo bado ipo katika jamii hizo kwani hiyo ilikuwa ndiyo tamaduni zao kwa miaka nenda miaka rudi.
Mwanakwetu kwa leo naishia hapo. Matini ijayo nitautazama utani wa Wajita na Wabaruli. Nakutakia siku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments