Header Ads Widget

CHAMISA - ARDHI YA TANZANIA INAZALISHA VIONGOZI WAZURI, ACT KUMPATA MRITHI WA MAALIM SEIF





Rais wa Chama Cha Upinzani nchini Zimbabwe Cha CCC, Nelson Chamisa amesema kuwa, ardhi ya Tanzania inazalisha viongozi wazuri wenye maono mengi kama aliyekua Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayyat Mwl Julias Nyerere ambayo yameleta mabadiliko Tanzania......Fatma Ally na Arodia Peter, MDTV Dar es Salaam



Kauli hiyo ameitoa leo, jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika Mkutano Mkuu Maalum wa ACT Wazalendo wa kuchagua viongozi wa Chama hicho, ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamo Mwenyekiti Zanzibar pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu .


Amesema kuwa,hakuna kiongozi anaetawala milele kiongozi wa hivo anakua tatizo, ambapo ameeleza kwa Afrika viongozi wazee hawataki kuachia madaraka, huku akisema kuwa chama chenye maendeleo kina vijana na wanawake.


Aidha, amekipongeza Chama hicho, kwa kuzindua Program ya ACT kiganjani  kwani dunia ya leo ni utandawazi hivyo, kuzinduliwa kwa program hiyo watakua wameenda ulimwengu unavyotaka.


"Afrika ni bustani hivyo, haipendezi kuwa na rangi moja, Bunduki sio gitaa hivyo sio kitu cha kucheza nacho, kwani bara hili linahitaji amani, Umoja  mshikamano Ili kuweza kufanya siasa nzuri na za kistaarabu"amesema Chamisa.



Kwa upande wake, Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe amesema mariadhiano ndio msingi mkubwa uliokijenga chama hicho, hivyo amewataka viongozi kuhakikisha wanakisimamia Chao.


"Licha ya mazila makubwa tuliyopitia katika kipindi cha uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020  ila tulisema tunakwenda kwenye meza ya mazungumzo na majadiliano, kwani bila mashirikiano hatuwezi kufika popote"amesema Zitto.


Aidha, amesema kuwa, wataheshimu sheria za haki ila hawatokua wastaarabu endapo haki zinazominywa, sambamba na kuwataka viongozi wa majimbo kuwa na maelewano mazuri na viongozi wenzao pamoja na wanachama Ili ikitokea wanahitajika wanachama hata saa tano usiku waweze kupatikana.


Naye, Naibu Msajili wa vyama vya siasa nchini, sisty Nyahoza akiwakilisha salam za Msajili wa vyama vya siasa Jaji France Mutungi amesema kuwa, amekuwa akishiriki mikutano mingi ya vyama vya siasa lakini ACT wamekua na siasa za ustaarabu sana.


Amesema kuwa, chama hicho, kimekua kikiheshimu na kutekeleza misingi ya demokrasia, huku akiwapongeza kwa namna wanavyokiendesha chama hicho ikiwemo  kufanya midahalo jambo ambalo limeleta taswira mpya kwa vyama vya siasa, huku akiwataka vijana kudumisha vyama vya siasa na utawala bora.


Akitoa salamu za wanachama wa ACT waishio nje ya nchi  (Dayaspora wa Uengereza), Mwenyekiti wa Vijana Taifa Abdul Nondo amesema kuwa, wanachama hao wanaumga mkono juhudi zinazofanya na chama chao, hivyo viongozi wowote watakao chaguliwa watawaunga mkono.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI