Header Ads Widget

SERIKALI KUWEKA ANUANI ZA MAKAZI KWA WANANCHI .

 



NA HAMIDA RAMADHANI DODOMA 




WAKATI tukiwa tumeuanza mwaka mpya 2022 Serikali imewataka wananchi,Ofisi na maeneo yote ya biashara yawe na anuani ya makazi jambo ambalo litasaidia na kurahisisha zoezi zima la Sensa ya watu na makazi ifikapo mwezi Augusti 2022 .


Hayo yamesema leo na Teddy Njau, kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari  kwenye semina ya kujenga uelewa kwa Viongozi na Watendaji wa Baraza kuu la Shirika la Posta Tanzania ambapo amesema kila moja anajukumu la kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.


Amesema utekelezaji wa zoezi la anuani ya makazi ni jambo mtambuka na unahusisha wadau mbalimbali ikiwemo wizara,Makampuni mashirika Taasisi serikali na zisizo za serikali na wananchi kwa ujumla. 


" Kwa kutambua hilo umeandaliwa mkakati wa utekelezaji unaoainisha majukumu ya kila mdau katika zoezi zima la utekelezaji wa mfumo huu ikiwemo shirika letu la posta Tanzania," amesema Njau


Aidha amesema mfumo huo una manufaa mengi katika dhama za ulimwengu wa digitali kurahisisha uapatikanaji na utoaji na ufikishaji wa huduma au bidhaa pale panapo stahiki kuwezesha kufanyika kwa bisahara za kimtandao kuimarisha ulinzi na usalama na kuongeza ajira.


Hata hivyo amesema ukamilishaji na utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi ni muhimu kwa kujenga ulewa na uwezo kwa wataalamu ili kuwe na uwezo wa kusimamia na kutekeleza mfumo huo.


"Yamefanyika mafumzo mbalimbali ya kujenga uelewa kwa pamoja juu ya umuhimu wa mfumo huo wa anuani ya makazi kwa wajumbe wa jumuia za serkali za mitaa ALAT,makatibu tawala wa mikoa pamoja na wakuu wa mikoa wote wa tanzania bara ili kwa pamoja kuweza kusimama kwa pamoja kutekeleza mfumo huu kwa ufanisi zaidi,"amesema Njau.


Aidha amesema kwa upande wa wataalamu wameweza kuwapa mafunzo  wataalamu wa tehama na maafisa mipango miji ramani kutoka Halmashauri zote nchini Tanzania Bara na Zanzibar ambapo walianzimia mpango kazi wa utekelezaji wa mfumo huo katika maeneo yao.


MAELEKEZO KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA BARAZA KUU LA SHIRIKA LA POSTA


Amesema ili kuboresha utendaji wa shirika viongozi hao wahakikishe wanaweka miundombinu za anuani ya makazi katika maeneo ya ofisi na majengo yanayomilikiwa na shirika la Posta,kuhakikisha wateja wa shirika wana anuani za makazi na wanazitumia ipasavyo,kuboresha mazingira ya ofisi ili kuruhusu huduma za posta na anuani kwa kutumia anuani za makazi, Kubuni huduma mpya kujitolea kuweka miundominu ya anuani za makazi katika maeneo ya makazi kama mabolozi .



Kaimu Posta Masta Mkuu kitendo Macrise Daniel amesema kitendo cha kuona munihimu na kuwashirikisha viongozi wakuu waposta katika mafunzo hayo ya mfumo wa anuani ya makazi ni muhimu kwa mustakabali wa taifa kwani itasaidia kurahisisha kazi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI