Uongozi wa Klabu ya Soka nchini, Simba Sport Club Wekundu wa Msimbazi ambao ni Mabingwa nchi wameweka bayana kuchukua jukumu la kugharamia matibabu kwa mashabiki wake waliopata ajali eneo Kahama, wakati wa kuelekea Mkoani Kagera kuitazama timu inayotarajia kucheza dhidi ya Kagera Sugar.
Simba anatarajiwa kushuka dimbani kucheza na Kagera Sugar Januari 26,2022 mchezo ambao ni wa kiporo kufuatia awali wachezaji wake karibu wote kushindwa kucheza kutokana na kuumwa mafua na homa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally alisema watagharania matibabu na huduma nyingine za kwa waliopata majeruha wakati wa ajali hiyo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Baadhi ya wanachama wa tawi la Wekundu wa Chalinze wametoa pongezi kwa uongozi wa Simba akiwemo Mtendaji Mkuu wake CEO, Barbara Gonzalenz.
0 Comments