Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi (AFDP) imetenga takribani sh Bil 29 mwaka 2022/2023 kwa ajili ya kuwezesha kiuchumi shughuli za uvuvi na mikopo kwa wananchi waliopo kwenye sekta hiyo pamoja na kukuza pato la Taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha mkakati na kampeni ya kuhamasisha shughuli za ukuzaji viumbe maji bahari kwa viongozi na wataalam katika Mamlaka za Serikali za mitaa mkoani Tanga.
Alisema kuwa sehemu ya fedha hizo takribani sh Bil. 2.1 zinakwenda kukopeshwa kwa vikundi vya wafugaji wa samaki, wakulima wa mwani,wafugaji wa majongoo bahari, wanenepeshaji wa kamba koche na kaa, katika ukanda wa bahari ya Hindi.
0 Comments