Header Ads Widget

TRC YAELEZEA MAFANIKIO YAKE

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema mwaka 2021 umekua ni mwaka wa mafanikio katika Sekta hiyo kwa kutoa huduma bora za usafiri kwa ndani na nje ya nchi.


Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam amesema Shirika hilo bado linaendelea kutoa huduma bora za usafiri kwa treni katika nchi jirani ikiwemo Kongo, Rwanda na Burundi kupitia Reli ya kati, na kuendelea na safari za treni kati ya Dar es Salaam, Tanga na Arusha na kusimamia vyema miradi ya ufufuaki na Ujenzi wa Reli mpya.


Amesema kuwa, Shirika hilo linatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam - Mwanza yenye vipande vitano, ikiwemo Dar es Salaam - Morogoro chenye jumla ya urefu wa km 300.


"Vipande vyengine ni Morogoro - Makutupora chenye jumla ya urefu wa km 422, Makutupora - Tabora chenye jumla ya urefu wa km 368, Tabora - Isaka chenye jumla ya urefu wa km 163 na Isaka - Mwanza chenye jumla ya urefu wa km 341"amesema Kadogosa.


Aidha amesema Shirika linatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya kwanza Dar es Salaam to Mwanza yenye vipande vitano ambapo hadi sasa inatekeleza vipande vinne ikiwemo cha Dar es Salaam- Morogoro kilichofikia asilimia 95 na Morogoro-Makutupora asilimia 77.


Hata hivyo, amewaomba wananchi na wadau kuendelea kutoa ushirikiano katika kulinda miundombinu ya reli kwa manufaa ya Taifa la Tanzania, huku akiwataka kuzingatia alama za usalama wa reli pindi wanapokuwa katika makutano ya reli na barabara kiwemo kusimamia umbali mrefu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI