Katika kukabiliana na upotevu wa maji haswa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyopelekea baadhi ya maeneo kukumbwa na ukame kiwanda cha sukari(TPC)kimeanza umwagiliaji kwa njia ya matone.Mwandishi Gift Mongi,Moshi
Njia hii ya umwagiliaji imeelezwa kuwa ni rafiki kwani inaokoa upotevu wa maji mengi ambayo hayatumiki katika mmea husika hivyo hupotea bure.
Meneja wa tume ya umwagiliaji mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Said Ibrahim alisema tayari wameanza kutoa elimu hiyo na kuwa TPC ambaye ni mkulima mkubwa wameanza kuitumia njia hiyo
"Tunashukuru kwa TPC kuanza kutumia teknolojia hii kwani itawawezesha kuweza kumwagilia kwa kipindi kirefu haswa wakati huu ambapo kuna uhaba wa maji kwenye baadhi ya maeneo" alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa chama cha wakulima na wafanyabishara(TCCIA)wilaya ya Moshi Louis Mbuya alisema njia hiyo ambayo imeanza kutumiwa na TPC mbali na kuwa rafiki kwa mazingira lakini itenda kuhakikisha upatikanaji wa miwa kwa msimu mzima wa uzalishaji.
Alisema TPC ni miongoni mwa kiwanda kikubwa mkoni Kilimanjaro na pia kimeajiri idadi kubwa ya wafanyakazi hivyo njia hiyo waliyoitumia ni sahihi katika kuona kuwa hawatasimama uzalishaji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Hii njia ambayo TPC wamekuja nayo itawezesha shughuli kuendelea bila kuathiriwa na hali ya hewa na pia kama kingesimama uzalishaji idadi kubwa sana ya watu wangeenda kuathirika" alisema
Naseeb Husein mkazi wa New land alisema teknolojia hii ni nzuri na kuwa ingefaa kutumiwa na wakulima wengine wakubwa ili kuendelea kuhifadhi maji yasipotee bila sababu za msingi.
Alisema kwa kipindi kirefu wakulima walio wengi wamekuwa wakitumia maji mengi katika kumwagilia wakati uhitaji kwa mmea ni kidogo jambo linalofanya maji kupotea bure.
Mwisho.





0 Comments