kamanda TAKUKURU mkoa wa Iringa,Domina Mukama akitoa taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi wa Takukuru mkoa wa Iringa mbele ya wanahabari (hawapo pichani)jana picha na Matukio Daima Media
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoni Iringa imethibitisha kumkamata Kwa askari wa usalama barabarani Copro Steven Mchomvu Kwa tuhuma za kwa kupokea rushwa Kwa madereva vya mbali mbali wakiwemo wa mabasi ya abiria .
Askari huyo picha zake zilisambaa kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuanzia juzi na kuzua maswali mengi zaidi ya wengi kutaka kujua ni tukio la mkoa gani .
"Pesa mlizoziona tulimkuta nazo mfukoni baada ya kumpekua zile kwenye gari tulizimwaga Kwa ajili ya picha na lile ni gari letu TAKUKURU"
Kwa mujibu wa Takukuru mkoa wa Iringa tukio Hilo lilitokea eneo la Ipogolo Manispaa ya Iringa kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya Januari 18 majira ya Saa 5 asubuhi mwaka huu .
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa kamanda TAKUKURU mkoa wa Iringa,Domina Mukama alisema kuwa TAKUKURU walimkamata Copro Steven Mchomvu akipokea rushwa kwenye mabasi ambayo yanapita katika barabara ya Iringa -Mbeya
Alisema kuwa picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zilipigwa na maafisa wa TAKUKURU mkoa wa Iringa mara baada ya kumkamata polisi huyo wa usalama barabarani akipokea rushwa kutoka Kwa madereva.
Mukama alisema kuwa mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa na taratibu zote zikikamilika atafikishwa mahakamani .
Hivyo alitoa onyo kwa watumishi wote wa umma kuacha mara moja tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa ni kinyume cha sheria za utumishi wa umma kama ambavyo walikula kiapo wanapoanza kazi.
Mukama alisema kuwa mara baada ya kumkamata askari wa usalama barabarani copro Steven Mchomvu alimshirikisha OCD wa Iringa kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa pamoja.
Aidha kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Iringa alisema kuwa wamefanikiwa kukagua jumla ya miradi kumi na mbili (12) yenye thamani ya shilingi bilioni saba milioni mia moja themanini na tano elimu mia tano sabini na tisa na kumi na tano (7,135,579,015).
Alisema kuwa miradi hiyo ni ya sekta ya elimu,ujenzi (barabara) na afya ambayo miradi hiyo ilikaguliwa kwa lengo la kujua thamani halisi ya pesa iliyotumika na na ubora wa miradi husika kama inaendana na miradi yote ilikaguliwa na kukuta inaendelea vizuri na kwa ubora unaotakiwa.
Mukama alisema kwa kipindi cha oktoba na disemba mwaka 2021 walipokea jumla ya malalamiko 48 yanayohusiana na rushwa lakini baada ya uchunguzi waligundua kuwa taarifa za rushwa zilikuwa 26 na 22 hazihusiani na rushwa.
MWISHO
0 Comments