Header Ads Widget

TAASISI YA DORIS MOLLEL FOUNDATION YASAIDIA MAPAMBANO YA MALARIA MASWA.

 







TAASISI ya Doris Mollel Foundation imetoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa malaria kwa wakinamama wajawazito na wanaonyonyesha katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.


Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Doris Mollel katika hospitali ya wilaya ya Maswa wakati wakitoa mafunzo ya umuhimu kwa wakinamama hao kujikinga na ugonjwa huo katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Uviko 19.


Amesema kuwa moja ya athari kubwa ya ugonjwa huo kwa wakinamama wajawazito ni kujifungua watoto kabla ya wakati  na hivyo kuzaa watoto njiti.


Ameongeza kuwa elimu hiyo itakayotolewa katika hospitali ya wilaya hiyo vituo vya Afya na Zahanati za wilaya hizo zitalenga kuwanusuru wakinamama hao ili wasiweze kushambuliwa na ugonjwa huo.


Hata Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa chini ya ufadhili wa Global  Fund wameweza kutoa vyandarua kwa ajili ya akinamama hao na watoto ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

              

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI