Header Ads Widget

RUZINGA DAY’ KUWA MFANO WAKUIGWA

 .



Wadau wa maendeleo kata ya Ruzinga Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera wamemshukuru mkurugenzi wa wilaya hiyo na serikali kwa ujumla kwa kuitazama kata hiyo kwajicho pana la kimaendeleo. Titus Mwandishi Mwombeki-MTDTV BUKOBA


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa sherehe ya ‘Ruzinga day’  Bi. Elizabeth Rugega wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambapo amesema kuwa wadau wa maendeleo katika kata yao wamejitahidi kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa nguvu zao lakini ofisi ya mkurugenzi wa wilaya hiyo imekuwa itoa ushirikiano sana walipokuwa wakitaka msaada kutoka kwao. 



“ Tumefanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika kata yetu sisi kama wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuweza kubomoa jengo la shule ya msingi Ruhija ambalo lilikuwa limechakaa sana na kuomekana kuwa hatarishi kwa wanafunzi na walimu na uweza kuanza ujenzi ambao unaendelea mpaka sasa, kuweka umeme katika shule ya sekondari Ruzinga,kuchangia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ruzinga, kununua vitanda kwaajiri ya kuwasaidia wanafuzi wa bweni pamoja na kukarabati wa madarasa yaliyoaribiwa na tetemeko” Alisema Rugega.


Aidha, amemuomba Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kuwasaidia kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba ya walimu pindi ujenzi huo utakapofikia katika hatua ya rinta.


Kwa upande wake diwani wa kata ya Ruzinga Rafiu Hussen  amemshukuru mgeni rasmi kwa kuitikia wito wa kuungana nao katika siku ya ‘Ruzinga day’ na kumuomba kuwapatia maganga wa mahabara katika kituo cha afya cha Ruzinga kinachopatikana katani hapo.


“Tulijitahidi sisi kama wadau wa maendeleo tukanunua darubini katika mahabara ya kituo chetu lakini chakushangaza mpaka sasa imepita miaka mitatu hatuna mtaalamu wa kutumia kifaa hiki jambo linalotuumiza sana, tuunaomba ofisi yako iweze kulitazama suala hili” alisema Rafiu.


Kwaupande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambaye pia ni mkurugenzi wa wilaya ya Misenyi Waziri Kombo ameupongengeza uongozi wa Ruzinga day pamoja na wadau wa maendeleo kwa kazi  nzuri za kimaendeleo  wanazozifanya na kuwaahidi kuwa ofisi yake na serikari kwa ujumla itakuwa bega kwa bega kuakikisha yote walioyaomba yanapatikana.


 “ Niseme kuwa serikali inapenda wananchi wajitoe ili wakishafika hatua Fulani serikali iweke nguvu zake ikiwa ni pamoja na kumalizia miradi hiyo binafsi naahidi fadha  zitaletwa katika kata hii kwaajiri ya kumalizia nyumba ya walimu na pindi mtakapofikia katika hatua ya rinta ikiwemo” alisema Kombo. 


Akitolea maelezo suala la ukosefu wa mtaalamu wa kutumia darubini katika kituo cha afya cha Ruzinga mheshimiwa Kombo amelisema kuwa suala hilo atalifanyia kazi na kuomba viongozi wa kata hiyo kuandika barua juu ya suala kwaajiri ya rejea.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI