Header Ads Widget

ROSE MUHANDO AMSHUKURU KUHANI MUSSA, AAHIDI KUFANYA MAKUBWA

Msanii wa nyimbo za injili nchini Tanzania Rose Muhando amesema amejipanga vyema kufanya mambo makubwa na watu watarajie mazuri kutoka kwake, kwani atakuja kivyengine.Mwandishi Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa shukurani kwa waumini na wafuasi wake wote wa nyimbo za injili ambao wamekua wakimkosoa na kumpa ushauri Ili afanye vizuri katika mziki wake.


 Amesema kuwa, mwaka 2021 ulikua mwaka mzuri kwake, ambapo ameweza kufanya mambo makubwa na mazuri katika kumtumikia Mungu, huku akiwashukuru watu wote waliofanikisha yeye kusimamia alipo kwa sasa.


Aidha, ameshukuru Mchungaji wa Kanisa la Fresh Spring Fellowship (Ngome ya yesu Kristo) Richard Mwacha kwa kumzawadia Gari Aina ya Toyota Prius, ambayo imemuomgezea hamasa sana katika kazi zake.


Amesema kuwa katika kipindi cha uimbaji wake cha miaka ishirini amekuwa akipitia vipindi vigumu lakini Mungu amemuheshimisha Mchungaji huyo kuwa saidia waimbaji ikiwemo yeye.


"Katika maisha ya uimbaji tunapitia mambo mengi lakini Kwa wachungaji tupotayari kupokea maonyo kutoka kwao, tuporadhi kukemewa na Wachungaji tuna wahitaji  sana'"ameema Rose Muhando.


Hata hivyo, amesema vyombo vya habari vimekuwa nguzo katika huduma yake ya Uimbaji na watu wote walichangia huduma hiyo.


Kwaupande wake, Meneja wa Muimbaji huyo Emanuel Mabisa amesema Rose Muhando amekuwa akipendwa na kupata kibali katika huduma yake ya Uimbaji katika nchi za Kenya, Ruwanda Burundi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI