Askari wa uwanja wa ndege katika kiwanja cha kimataifa cha kilimamjaro wametakiwa kutoa huduma bora kwa watumiaji wa uwanja huo ambao ni lango kubwa la utalii
Kamanda wa polisi wa viwanja vya ndege nchini, Jeremiah Shilla ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea uwanja huo na kuzungumza na askari wa kituo kidogo cha polisi KIA na kukagua makazi yao.
Amesema askari wa KIA wanapaswa kushirikiana na vyombo vingine kutoa huduma bora ikiwepo kwa watalii wanaotumia uwanja huo.
Kamishna Shilla pia ameagiza polisi katika uwanja wa ndege wa kimataifa kilimanjaro(KIA) kudhibiti dawa za kulevya katika uwanja huo.
Amesema nilazima polisi waongeze bidii katika kukabiliana na madawa yakulevya katika uwanja huo, kwani bado kuna madawa mitaani.
Awali Mkuu wa kituo kidogo cha polisi KIA, Edith Makweli amesema polisi KIA wanafanyakazi vizuri.
Amesema kwa kushirikiana na vyombovingine wameweza kudhibiti uhalifu katika uwanja huo ikiwepo dawa za kulevya.
Kamanda Shilla kesho anatarajiwa kuzungumza na wanaotoa huduma za usafiri katika uwanja huo,kutembelea KIA na kuzungumza na wadau wa uwanja huo.





0 Comments