Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam.
Wasomi kutoka jamii ya wafugaji waishio wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya wafugaji na wahifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro.
Wakizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam wasomi hao, wamesema wamekua wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo mlipuko wa njaa, magonjwa yanayoambikwa na yasiyoambukiza kutokana na ukosefu wa lishe bora pamoja na kushindwa kufanya shughuli za kijamii.
Aidha wamedai kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikifanya kampeni ya kuwaondoa wafugaji hao kwa madai kuwa wanaharibu hifadhi ya Ngorongoro jambo ambalo si kweli kwani wamekua wakiishi hapo kwa muda bila kuleta athari yoyote.
Laata Mekusi Msomi Chuo Kikuu Mzumbe ambae ni miongoni mwa wazungumzaji, ameiomba Serikali itambue kuwa eneo la kilometa za mraba 1,500 linalodaiwa kuwa litakuwa pori tengefu, eneo hilo lina maslahi na wananchi kwani ndipo vilipo vyanzo vya maji na malisho kwa ajili ya mifugo na itambulike kuwa ufugaji ndio rasilimali pekee ya wananchi wa loliondo.
"Tupo tayari kukaa meza moja na Serikali kwa ajili ya kujadili suala hili, na hata kuboresha hifadhi hii, ila hatutaki kuondoka kwani ile ardhi ndio tunaitegemea katika kuendeshea maisha yetu"amesema.
Msomi Chuo kikuu cha SUA Megoliki Meng’oru pamoja na Selina Mungaya ambaye ni Msomi chuo kikuu Mzumbe wameishauri Serikali iwashirikishe wadau wote wa Loliondo katika mchakato wa kutatua mgogoro huo na kuzingatia yafuatayo
Naye Ezekiel Ole Mangi ni Msomi jamii ya wafugaji amesma mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanachi hawajawahi kuwa tatizo kwa wanyama wala uhifadhi kwa ujumla ila ni sera na sheria ambazo zimekuwa ni kikandamiza kwa maisha yao.
Hata hivyo, amesema ni wakati muafaka kuandaa mjadala juu ya kurekebisha sera na sheria zilizopitwa na wakati hasa zinazokandamiza utu na kukiuka haki za binadamu.
Aidha wasomi hao wamesema kuwa kutekeleza dhana inayofikiriwa na wahifadhi ya kuunda Ngorongoro mpya kuwaondoa jamii ya wafugaji katika hifadhi hiyo itapoteza uhalisia wa uanzishwaji wa hifadhi ya Ngorongoro.
Mapema mwaka huu, Jan 25, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC Onesmo Olengurumwa wakati akizungumza na wanahabari akitoa taarifa ya hali ya utetezi wa Haki za Binadamu katika migogoro ya Ardhi Wilayani Ngorongoro alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuwapa nafasi na kuwasikiliza wananchi wa Loliondo ili kusikia hoja zao na hatimaye azifanyie kazi ili mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
0 Comments