Uongozi wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi RDO Mdabulo na RDO Kilolo vinavyo milikiwa na Shirika la Rural Development Organization (RDO) unawatangazia nafasi za mafunzo ya Ufundi Stadi kwa mwaka wa masomo 2022. Vyuo pia vinaendelea kupokea wanafunzi wa kozi fupi kwa muda wa miezi mitatu na miezi sita.
Kozi/Fani zitolewazo vyuoni ni:-
1. Umeme wa Majumbani na Viwandani (Electrical Installations),
2. Upishi (Food Productions),
3. Uchomeleaji na Uundaji Vyuma (Welding and Metal Fabrications),
4. Uashi (Masonry and Bricklaying),
5. Useremala (Carpentry and Joinery),
6. Ubunifu wa Mitindo ya Mavazi na Ushonaji (Design, Sewing and Cloth Technology/Tailoring),
7. Mifugo (Animal Husbandry),
8. Nishati Jadidifu (Renewable Energy)
9. Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fittings) na
10. Kompyuta (Computer Applications)
Vyuo vimesajiliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). RDO Mdabulo kwa namba *VET/IRA/FR/2020/C/115* na RDO Kilolo kwa namba *VET/IRA/PR/2019/C/106.*
Fomu za kujiunga na vyuo zinapatikana maeneo yafuatayo bure;
Chuoni RDO Mdabulo, RDO Ibwanzi na RDO Kilolo,
Kituo cha RDO Mafinga-Kinyanambo,
Kituo cha RDO Malangali na
Village Centres Isele, Ludilo, Nandala, Mapanda, Itona na Mpanga TAZARA.
Nafasi za bweni kwa waombaji wote zinapatikana. Karibu RDO Mdabulo VTC na RDO Kilolo VTC kwa Mafunzo na Malezi Bora.
Kwa maelezo zaidi, Wasiliana nasi kwa:-
Simu:- 0757 351 837 / 0752 251 568 / 0765 488 567
Ufundi ni Taaluma Inayoishi
0 Comments